FAHAMU JINSI MAMILIONI YANAVYOTUMIKA ILI KUPANGA MATOKEO YA SOKA

FAINALI za Kombe la Dunia zitakazofanyika Brazil mwakani zipo kwenye hatari kubwa ya kukosa mvuto. Ni kwa sababu kuna baadhi ya mechi matokeo yake yatapangwa na wacheza kamari, imeelezwa.

Wiki iliyopita watu sita walitiwa nguvuni kwa madai ya kushiriki kwenye kucheza kamari za kupanga matokeo ya mechi za soka na mmoja wa watuhumiwa hao alifichua kwamba mipango imeshawekwa tayari kwa ajili ya fainali zijazo za Kombe la Dunia na kwamba timu zote za Afrika zilizofuzu fainali hizo zipo kwenye himaya yake.

Timu za Afrika zilizofuzu ni Ghana, Ivory Coast, Nigeria, Cameroon na Algeria.

Hii ina maana kwamba atajipangia matokeo na mambo anayotaka yatokee kwenye mechi zao ili kushinda mamilioni ya kamari anayocheza.

Kwenye orodha ya waliotiwa nguvuni ni straika wa zamani aliyetesa kwenye Ligi Kuu England, Delroy Facey, ambaye kwa sasa ni wakala wa soka.

Facey, 33, aling’ara katika timu za Bolton Wanderers na Hull City zilipokuwa kwenye Ligi Kuu England kabla ya kufanya shughuli za uwakala wa soka.

Watu wengine waliokamatwa kwa kupanga matokeo ni Chann Sankaran, 33, kutoka Singapore na Krishna ­Ganeshan, 43, mwenye uraia wa nchi mbili; Uingereza na Singapore.

Wote walitarajiwa kufikishwa mahakamani jana Ijumaa. Kwa maelezo ya watu hao, Asia imeathirika zaidi kuwa na idadi ya watu wengi wanaoshiriki kwenye kupanga matokeo ya mechi za soka zinazochezwa duniani kote.

Kamari za upangaji wa matokeo ni virusi vinavyoishambulia soka kwa kiwango kikubwa kutokana na kuwashirikisha wahusika wenyewe kuanzia wamiliki wa timu, wachezaji, waamuzi na mawakala wa Shirikisho la Kimataifa la Soka (Fifa) wanaohakikisha wanatengeneza njia nzuri za mawasiliano ili kupanga matokeo ya mchezo.

Mambo yanavyofanyika

Kwa mujibu wa maelezo ya mtu huyo aliyenaswa, ni kwamba kinachofanyika katika kupanga matokeo kwa baadhi ya timu za klabu, wamiliki wake wamekuwa wakipigiwa simu usiku wa kuamkia siku ya mechi na kupewa maagizo kwamba lazima wafungwe kwenye mechi yao, huku hongo zikifanyika pia kwa makipa ili wafungwe kinafiki, mabeki wasababishe penalti kizembe kwa kushika mpira kwa makusudi huku mabao mengi ya dakika za mwishoni mwa mchezo yadaiwa kutokana na michezo hiyo ya kamari.

Kuna kundi jingine pia linalowahusisha wachezaji moja kwa moja wanaojiingiza kwenye upangaji wa matokeo kwa sababu jambo hilo linawaingizia pesa za ziada ukiacha mishahara yao na bonasi nyingine.

Nchi zinazoathirika

Ligi Kuu England kinachoinusuru ni mishahara mikubwa wanayolipwa wachezaji, lakini kwa nchi kama za Ubelgiji, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Finland, Sweden na nchi mbalimbali za Afrika kuna wachezaji wanaoshawishika kirahisi na kukubali kucheza kamari hizo za kupanga matokeo.

Vikundi vinayojishughulisha na kamari hizo za kupanga matokeo vimekuwa vikitengeneza mazingira ya kuwasiliana na wachezaji, makocha au waamuzi ili kuhakikisha wanafanya kile wanakitaka wao ikiwa pamoja na kutoa kadi za njano, kadi nyekundu, kutoa penalti au kuhakikisha mechi husika inamalizika kwa matokeo ya sare.

Kadi ya njano yanunuliwa Pauni 5,000

Kwenye kamari hizo, kadi za njano zinazotoka ndani ya dakika 10 za kwanza kwa mchezaji ambaye alikubali kufanya tukio hilo zinamhakikishia mhusika kulipwa Pauni 5,000.

Lakini, mtu anayejihusisha na kamari hizo anasema kama mchezaji husika atashindwa kufanya tukio litakalomfanya aonyeshwe kadi ya njano ndani ya dakika 10 za mwanzo, basi atakuwa amepoteza nafasi ya kulipwa pesa hizo na hata kama ataonyeshwa kadi baada ya dakika hizo kupita, atakuwa yupo nje ya makubaliano.

Anasema: “Kwa mfano, ndani ya dakika 10 kama nitataka mchezaji aonyeshwe kadi ya njano na kadi moja ya njano thamani yake ni Pauni 5,000.

Hivyo ndivyo nilikuwa nikipanga na wachezaji. Kama hakutakuwa na kadi ya njano dakika hizo, hakuna malipo.”

Pauni 20,000 zanunua waamuzi

Kiasi cha Pauni 1.73 milioni zinatajwa kutumika kuwahonga wanaotumika kwenye kupanga matokeo kwa Ujerumani peke yake, wakati wachezaji kwenye nchi za Uingereza wamekuwa wakihitaji Euro 60,000 ili kukubali kucheza kamari hizo.

Kwa maelezo yaliyopatikana ni kwamba Pauni 20,000 zinatumika kumnunua refa anayechezesha mchezo husika ili apange matokeo wanayoyataka yaliyopangwa kwenye kamari zao, kwa mfano kwamba lazima mchezaji fulani aonyeshwe kadi ya njano au nyekundu.

Mwamuzi wa Armenia, Andranik Arsenyan, alifungiwa maisha baada ya kugundulika kujaribu kupanga matokeo ya mchezo wa Europa League wakati mwaka 2010, mwamuzi wa Bosnia, Novo Panic, pia alifungiwa maisha. Chann Sankaran na Krishna Sanjey Ganeshan, walitiwa mbaroni kwa kudaiwa kupanga matokeo kwenye mechi za England.

Serie A yachafuka zaidi

Wakati timu za Afrika zikidaiwa kuwekwa kwenye mchakato wa kupanga matokeo kwenye fainali zijazo za Kombe la Dunia zitakazofanyika Brazil mwakani na kutishia kupunguza uhondo wa michuano hiyo, Ligi Kuu Italia (Serie A) inaripotiwa kuchafuka zaidi kwa upangaji matokeo.

Ukiacha kashfa ya Calciopoli iliyosababisha Juventus kushushwa daraja mwaka 2006 kutokana na kupanga matokeo, lakini soka la Italia linaonekana kuoza kwa upangaji wa matokeo kwa sababu tukio hilo liliripotiwa kutokea tena mwaka 2011.

 Februari mwaka huu, BBC Sport ilitoa ripoti iliyoshitua wengi kwamba zaidi ya mechi 680 za soka duniani kote zimepangiwa matokeo, ikiwamo za Ligi ya Mabingwa Ulaya zilizofanyika England kati ya mwaka 2009 hadi 2013.

Zaidi ya nusu ya mechi hizo ni za Ulaya, huku Afrika na Asia ni mechi 300 zilizopangiwa matokeo.

Ugumu wa kuzuia jambo hilo ni kwamba pesa nyingi zimekuwa zikitumika kuwapa ofa wahusika ili washiriki na hivyo kusababisha vita hiyo kuwa si rahisi kuizuia.
Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. balaaaaaaaaaa ilooo.....

    ReplyDelete
  2. Illuminati ize work brooH

    ReplyDelete
  3. chanzo cha hiyo habari???????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad