TASNIA YA BONGO MOVIES CHALI-KANUMBA ALIONDOKA NA KILA KITU-SASA WAMEBAKI KUHAHA NA KUBADILI FANI

Je ni kweli Steven Kanumba ameondoka na Kila kitu?
Tangu Alipofariki Tasnia ya filamu Tanzania ni kama imelala usingizi wa Pono, Potelea mbali hata kama kuna watu bado wanaingiza mamilion ya pesa lakini ukweli ni kwamba mvuto wake unaendelea kupotea ..Nani anabisha?

Kwa kudhihirisha hilo Tazama wasanii wa kike wanavyojiingiza kwenye fani zingine zinazolipa ..Hawataki tena kupaka poda za location bali wanataka kukata viono kama Ray Majukwaanii...Mabadiliko na Maisha ya Shilole na Snura ni Mfano Tosha kabisa..

Kanumba alikuwa ni kila kitu biashara ya Filamu ilifanyika kupitia yeye..mzunguko wa soko uliundwa kupitia kanumba..Alisafiri kutoka mashariki kwenda magharibi, kaskazini na kusini kwa sababu ya tasnia ya filamu tu hakuwa akisafirisha Unga wala Pembe za ndovu..
Hivi sasa wasanii wa filamu hawavumi kupitia kazi zao, Ukimtazama mtu kama Ray utagundua kazi zake zilikuwa zinavuma kwa msukumo wa Ray lakini sasa zote chali ...Sasa anavuma kwa kugonganisha vimwana badala ya kuingiza movies mpya mtaani...

Kinacho Imaliza Bongo Movies kwa sasa ni Ubinafsi, Haraka , Mipango Butu na Tamaaaaa....

This is Wake up Call...

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. hapo ndo utakapojua kanumba aliwabeba kiasi gani, ndo ivo jembe kaondoka tutafanyaje

    ReplyDelete
  2. ni kweli kabisa

    ReplyDelete
  3. Yenyewe bana.. Kanumba was the greatest.. Hata bongo film za sasa si tamu kama za marehem.. RIP Steve.. Sad..:-(

    ReplyDelete
  4. R.I.P KANUMBA pengo lako halitazibikaaaaaaa...

    ReplyDelete
  5. Waliobaki nikuendekeza ngono tu.Wiviu,chuki ndio mtaji wao.Hawana ubunifu wowote zaidi

    ReplyDelete
  6. tangu kanumba afe sijawahi kununua cd yeyote ya bogo move maana ni urojo tuuu

    ReplyDelete
  7. Umeongea ukweli mtupu, uncle jj toka aondoke na bongo muv imekufa na sasa ipo inasahaulika

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad