Facebook, Twitter na Instagram ndio mitandao ya kijamii inayotawala maisha ya mtandaoni kwa watu wengi duniani. Hadi sasa Facebook ina watumiaji bilioni 1 duniani kote, Twitter ikiwa na watumiaji milioni 250 na Instagram ikiwa na watumiaji milioni 150.
Hata hivyo, takwimu zinazonesha kuwa Instagram inakua haraka zaidi kuliko Twitter na utumiaji wake kwa sasa ni mkubwa kuliko Twitter. Ikumbukwe kuwa vita kati ya Twitter na Instagram ilianza December mwaka jana baada ya Instagram inayomilikiwa na Facebook, kuacha kushirikiana na Twitter.
Kabla ya hapo, watu walikuwa na uwezo wa kuona picha za Instagram kirahisi kupitia Twitter hivyo Twitter ilikuwa inapata watumiaji wengi Instagram. Baada ya urahisi huo kuondelewa, watumiaji wengi wa Twitter wamejikuta wakiitumia zaidi Instagram.
Kwa mujibu wa ripoti, Twitter inapata shida zaidi kwa kupigwa chini na Instagram ambayo imeendelea kuneemeka tu. Kuna ubadilishanaji picha wa asilimia 59 tu kwenye Twitter ukilinganisha na asilimia 98% kwenye Facebook.
Tangu Instagram iache kusupport picha kwneye Twitter, mtandao huo umepata pigo kubwa kwa kupungua kwa matumizi ya picha huku Instagram kwa upande mwingine ikiendelea kukua ambapo ongezeko la followers limefika 41%.
Kwa utafiti wa kawaida tu na hata hapa Tanzania, utagundua kuwa kumekuwepo na watumiaji wengi mno wa Instagram.
Mastaa wa Tanzania wameonekana kuvutiwa zaidi na kuwa ‘active’ kwenye mtandao huo kuliko Twitter wala Facebook.
Kuna mastaa wengi ambao huwezi kuwaona Facebook wala Twitter lakini wako active zaidi Instagram. Kwa mfano kuna waigizaji wachache sana wa filamu Tanzania wanaotumia mtandao wa Twitter lakini wakiwa na followers wengi Instagram.
Sababu kubwa zinazochangia Instagram kupendwa zaidi ya Twitter na Facebook kwa mazingira ya Tanzania ni ule urahisi wa kuweka picha nyingi bila ulazima wa kuweka maelezo mengi na ile imani kuwa picha huongea maneno mengi kuliko maandishi kama ilivyo kwenye Twitter na pia Facebook ikiwa imetawaliwa na watu aina mbalimbali wakiwemo wakorofi na wanaopenda kutukana watu.
“Mi naweza kusema kwamba Instagram ni sehemu unayoweza kuona how crazy stars can be,” anasema Wema Sepetu kujibu swali la kwanini anapenda kutumia zaidi Instagram kuliko Twitter. “Watu wengi ambao nawafollow on Instagram ni macelebrities wa nje. So I follow people like Ellen Degeneres, I follow Soulja Boy, I follow 50 Cent, I follow Kim Kardashian, I follow the Kardashians, Nicole Ritchie, Rihanna. This is the only place ambayo ninaweza kuwaona how crazy they can get, it’s kila mtu amekuwa an ‘Instagram freak’ right now. Through profile ya mtu ya Instagram, unamjua mtu alivyo. It’s very hard to tell from Twitter cause it’s just mtu anaandika tu, ‘sasa hivi niko wherever’ anaweza akadanganya. Lakini kwenye Instagram, you can actually tell ‘Yeah nimeenda sehemu fulani nimepiga picha I’m here, nimepiga picha chakula changu, I am eating’ it’s just interesting.”
Kwa upande wake muigizaji wa filamu, Irene Uwoya anaamini kuwa mtandao wa Facebook ni kama daladala ambako kuna fujo za kila aina na ndio maana anaipenda zaidi Instagram kwakuwa watuamiji wake wengi ni waelewa.
“Facebook imechafuka sana,”anasema. Matusi, watu waandika vitu vya ajabu yaani changanyikeni, kila mtu yupo Facebook. Naweza nikatolea mfano kama usafiri, basi Facebook ni daladala. Instagram ni latest, kama ni gari basi ni Range new model, kama langu. Watu wanaoingia Instagram ni watu wa ukweli, watu wanaoingia huko ni wenye akili zao timamu, japokuwa kuna wachache waliotoka huko huko kwenye Facebook wanakuja kuchafua Instagram.
Irene anasema maudhi ya Facebook yalimfanya ajiondoe muda mrefu uliopita na wala hana akaunti tena.
“Kuna watu wanajifanya mimi sasa kwenye Facebook, wakati mimi sipo Facebook toka siku nyingi. Kuna akaunti kama saba za kwangu kila mtu ananiambia ‘nimekutumia meseji Facebook’ nawaambia ‘bwana mimi Facebook nilishatoka.”
Kwa upande wa Jokate Mwegelo, Twitter, Facebook na Instagram yote ni mitandao muhimu kwake.
“Mimi kotekote. Twitter napenda zaidi kuongeza mambo ya current affairs etc. Instagram picha zaidi na Facebook natoa mawaidha,” anasema.
Hata hivyo wataalam wanasema ingawa namba zinaonesha kuwa ni vizuri kuitegemea Instagram kwa sasa, watumiaji wa mtandao hawapaswi kusahau kuwa vitu vingine muhimu vinavyofanywa na Twitter. Mtandao huo hutoa vifaa zaidi ya kusambaza picha. Kwa biashara na watumiaji wa kawaida kuweza kuwafikia vizuri walengwa wao, wanatakiwa kupitia tena mikakati yao kwa kuchunguza mitandao mbalimbali ya kijamii kwa matumizi yanayofaa.
Pamoja na watu wengine kuanza kuikimbia Facebook kwa kuwepo na watu wengi wanaoitumia vibaya, bado imeendelea kuwa jukwaa muhimu linalotumiwa na makampuni, mashirika, viongozi na watu mashuhuri kuwasiliana na wateja ama mashabiki wao kwa haraka na kwa njia inayowafikia watu wengi.
-Bongo.com
JE WAJUA KUWA INSTAGRAM INAKUWA HARAKA KULIKO TWITTER..MASTAA WA BONGO INSTAGRAM NDIO HABARI YA MJINI
0
December 12, 2013
Tags