KINANA AIBOMOA NGOME YA CHADEMA

Mzimu wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kuwavua uongozi; Dk Kitila Mkumbo, Zitto Kabwe na Samson Mwigamba umeendelea kukitafuna chama hicho baada ya Katibu wa chama hicho Wilaya ya Chunya, Bryson Mwasimba kuvua gwanda.

Hatua ya kiongozi huyo imekuja ikiwa ni siku mbili baada ya Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Lindi, Ally Chitanda kutangaza kujiondoa katika nafasi hiyo akieleza kuchoshwa na uamuzi wa kikanda na kikabila unaoendelea ndani ya chama hicho.

Mbali na Uenyekiti, Chitanda pia alikuwa Mjumbe wa Baraza Kuu la Taifa na Katibu Ofisi ya Katibu Mkuu- Sekretarieti nafasi ambayo pia alitangaza kujiuzulu jana, lakini akaahidi kuendelea kuwa mwanchama mwaminifu wa Chadema.

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika wilayani Chunya chini ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na timu yake, Mwasimba alisema: “Sasa nataka kuungama dhambi nilizowafanyia ndugu zangu wakati nikiwa Chadema.

“Niliwadanganya mengi nanyi mkaniamini. Sasa naungama kwenu mnisamehe, lakini mfahamu kwamba wenye lawama kubwa ni Chadema kwa sera zao za kuhimiza wanachama na viongozi wake kuwa waongo na malengo ya ovyo.

“Pili; nilihamasishwa kufanya vurugu katika Kijiji cha Saza, sasa ikawa mimi na wenzangu 14 tukafungwa Gereza la Luanda.

“Sasa kabla sijaendelea kusema yaliyo safi naomba kwanza nilivue gwanda hili la Chadema najuta kulivaa tangu 2008, huu naona ni mkosi kwangu,” alisema Bryson, akiwa jukwaani huku akishangiliwa.

Baada ya hapo vijana wa CCM walimvalisha shati la kijani na kuhutubia halaiki ya wanaCCM akisema ni kati ya vyama vyenye sera, mlengo na kufuatilia utekelezaji wa ilani na ahadi zake.

Awali Katibu Mkuu, Kinana aliwahakikishia wakazi wa Chunya kwamba Serikali itakamilisha ujenzi wa barabara ya lami kutoka Mbeya hadi Chunya. Leo Kinana anatarajia kuwasili wilayani Mbarali.

Naye Msemaji wa Chadema, Tumaini Makene alisema katika taarifa yake jana kuhusiana na kujiuzulu kwa Chatanda: “Kwanza suala la uamuzi wa Kamati Kuu ya kuwavua uongozi ndani wa chama, Zitto Kabwe na Dk Kitila Mkumbo, mjadala wake kwa upande wa chama umeshafungwa, huku taratibu za kikatiba za ndani ya chama zikiendelea.
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. mtashaaaaaa sijui mtawadanganya nn wanachama wa chadema

    ReplyDelete
  2. ccm mafisad,cdm wababaishaji,ukabila na ukanda,sasa sijui tunafanyaje

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad