KATIKA kuhakikisha kikosi chake kinafanya vizuri kwenye mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara, kocha mpya wa Simba, Zdravko Logarusic amesema ataweka sheria kali zitakazowabana wachezaji wake juu ya vitendo vya utovu wa nidhamu.
Logarusic raia wa Croatia ambaye jana Jumatatu alisaini mkataba wa miezi sita kuifundisha Simba, aliliambia Mwanaspoti kuwa hakuna soka la ushindi bila ya nidhamu na anajua tabia za wachezaji wa Kiafrika ndiyo maana ameamua kuwatungia wachezaji kanuni hizo.
Kocha huyo alisema hazitakuwa kanuni kali ambazo zitaogopesha wachezaji lakini ni moja ya taratibu zake za kufundisha katika klabu yoyote anayofanyia kazi.
“Najua tabia za wachezaji duniani kote, lakini kwa Afrika nina uzoefu zaidi muda wowote unapotaka mafanikio katika timu lazima nidhamu iwe ya hali ya juu, bila ya hivyo hakuna utakalofanya.
“Kabla ya kuanza mazoezi nitawapa wachezaji sheria ambazo hawapaswi kuzivunja ili kuifanya timu iwe na nidhamu na kuwa mfano katika ligi, sheria hizi zitawafanya wawe makini ndani na nje ya uwanja,” alisema Logarusic mwenye umri wa miaka 51.
Alisema unapoendesha timu kwa misingi ya sheria ambayo kila mchezaji na mtendaji mwingine wa klabu ataifuata inakuwa rahisi kutimiza malengo ya kufanya vizuri uwanjani na hata kutwaa ubingwa.
Msimu huu aliyekuwa Kocha wa Simba, Abdallah Kibadeni mara kadhaa alikuwa akilalamika kuhusu utovu wa nidhamu kwa baadhi ya wachezaji wake na aliwahi kutofautiana na kiungo wake Henry Joseph.
Katika hatua nyingine Logarusic alisema hamjui mchezaji yeyote wa timu hiyo, hivyo kila mchezaji anapaswa kujituma ili acheze kikosi cha kwanza.
Alisisitiza kuwa hawezi kutumia kikosi cha kwanza cha kocha aliyepita, yeye anaanza upya kupanga kikosi chake.
Hiyo huenda ikawa dalili njema kwa wachezaji wa timu hiyo ambao walikuwa hawapangwi mara kwa mara na kocha aliyetimuliwa Abdallah ‘King’ Kibaden.
Baadhi ya wachezaji waliokuwa na wakati mbaya kwenye utawala wa Kibadeni ni Ramadhan Chombo’Redondo’, Amri Kiemba na Edward Christopher.
Logarusic aliliambia Mwanaspoti kuwa wachezaji wote wa Simba wana nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza na ataanza rasmi kazi ya kutafuta kikosi cha kwanza katika mazoezi yaliyotarajiwa kuanza jana jioni kwenye Uwanja wa Kinesi.
alichokikuta japokuwa kuna vitu vya kuanzia ambavyo anataka kuvifanyia kazi.
Kocha huyo alisema ili mchezaji apate nafasi ya kudumu katika kikosi cha kwanza anapaswa kuonyesha kiwango cha hali ya juu sambamba na nidhamu nzuri kwa kila mtu ndani ya timu
Tunakutalia mafanikio mema wanwamsimbazi
ReplyDeleteHizo mbwembwe tushazizoea sana walikuepo wengi kabla yako ambao kama wewe walikuja kwa kasi lakini mwishowe hawakuita hata press conference kuwaaga kila la heri ktk kazi ngumu kuliko zotr Tz kufundisha mpira kwani kila mwanachama
ReplyDelete, shabiki, kiongozi, wachezaji na n.k wote ni makocha kazi kwako