Lakini huwezi kuongelea tarehe 27 April 1974, siku ambayo Manchester United ilishishuka daraja, bila kumwongelea Denis Law. Denis Law ni legend Old Trafford. Alijiunga na Manchester United mwaka 1962 akitokea Manchester City. Aliichezea Manchester United kwa muda wa miaka 11, ambapo alifunga magoli 237 kwenye mechi 404 alizocheza. Mashabiki wa Manchester United walimwita “The King” na “The Lawman”.
Itakumbukwa pia kuwa Manchester United ilikuwa ikisuasua kwenye ligi baada ya timu kupata ajali ya ndege Munich Ujerumani mwaka 1958 ambapo abiria 20 kati ya 44 walipoteza maisha. Kati ya abiria 20 waliofariki, saba walikuwa wachezaji wa Manchester United. Kwa hiyo, baada ya ajali hiyo, Manchester United ilikuwa wanapambana mara nyingi kuepuka kushuka daraja.
Baada ya kuichezea Manchester United kwa miaka 12, Denis Law alihamia Manchester City msimu wa 1973/74 bila ada (free transfer). Manchester United walikuwa hawamhitaji tena maana kiwango chake cha mpira kilikuwa kimeshashuka na umri pia ulikuwa umesogea. Pia George Best na Bob Chalton walikuwa wameshaondoka.
Katika mechi ya mwisho ya ligi msimu wa 1973/74, Manchester United ilicheza na Manchester City Old Trafford. Manchester United ilitakiwa kushinda ile mechi ili isishuke daraja. David Law alicheza lakini tokea mwanzo alionekana kutokuwa na raha maana kama timu yake kipenzi (Manchester United) ingefungwa basi ingeshushwa daraja.
Mpaka dakika ya 80 mechi ilikuwa bila bila. Mnamo dakika ya 81, Denis Law aliifungia Machester City goli kwa kisigino. Lilikuwa goli zuri na tamu lakini siyo kwa mshabiki yoyote wa Manchester United. Denis Law mwenyewe hakushangilia kwa kufikiri kuwa goli lake la kisigino lingeishusha daraja Manchester United. Mara tuu baada ya kufunga like goli, alibadiliswa huku akitoka uwanjani akiwa ameinamisha kichwa chini kwa masikitiko makubwa ya kuishusha daraja Manchester United.
Baada ya Denis Law kutoka uwanjani, mashabiki wa Manchester United walivamia uwanja na kumlazimisha refa kumaliza mechi katika dakika ya 85. Siku chache baadae, chama cha mpira kilifanya mapitio ya mechi ile na kusimama na matokeo ya mechi. Kwa hiyo, Manchester City ikawa imeshinda bao moja lililofungwa na Denis Law kwa kisigino na Manchester United kushushwa daraja.
Hata hivyo, ilikuja kugundulika baada ya mechi kuwa bado Manchester United ingeshuka daraja bila kutokana na matokeo ya ile mechi. Hii ilitokana na matokeo ya kwenye mechi nyingine za mwisho zilizochezwa siku ile. Lakini Denis Law aliamini kabisa kuwa goli lake la kisigino limeishusha daraja Manchester United.
Msimu uliofuata (1974/75) Manchster United ilicheza kwenye ligi ya daraja la pili na kufanikiwa kurudi tena ligi ya daraja la kwanza katika msimu wa 1975/76.
Watch Video:
Itanambia nn man u mm imefulia msimu huu had aibu kuitamka
ReplyDelete