Akiongea bungeni leo, Bi. Rukia amesema Brigitte Alfred hafai kuiwakilisha Tanzania kwakuwa hawezi kuzungumza Kiswahili. Mbunge huyo alienda mbali zaidi kwa kupendekeza mashindano ya Miss Tanzania yafutwe na badala yake yawekwe mashindano ya Sayansi kwa manufaa ya taifa.
Akijibu kauli hiyo, Brigitte amesema: Meanwhile as our county suffers from 3rd world problems this is what is being discussed bungeni. I would love to meet this this woman! Asante mama,” ameandika mrembo huyo kwenye Instagram. “All of your comments give me hope that there’s still sensibility out here,” aliongeza.
“Mh.Rukia amekosa mada bungeni?*rollingmyeyesoutloud*,” alitweet.
“Anko in the office must be jumping for joy right now-they love to say ‘I told you so’-In Kiswahili ofcourse.”
Hata hivyo Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara alisema serikali haiwezi kuyafuta mashindano hayo kwakuwa yana umuhimu mkubwa kwa taifa na yamekuwa yakiitangaza nchi na shughuli za utalii.
Miss tanzania mzima hajui lugha yake ya taifa majanga haya!
ReplyDeleteWatu watamponda huyu mbunge bt ana point kubwa sana, huyo brigitter aache mapozi ya kisenge kujua kimombo sio issue mbona cku hizi jata chekechea wanaongea, kinachotakiwa kwa miss tz ni lazima ajue kiswahili fsaha hata kama anajua kijerumani pia, jamani watz whats kimombo mbona kawaida sana? mnampaisha mtu kwavkuongea kizungu tu basi.
ReplyDeleteHuyu Bibi wa kipemba kaongea neno nalo...hao ma Miss kazi kutuaibisha tu hawana lolote.
ReplyDeleteNilimsikia alipokuja bungeni na NGO ya Under the same sun. Kweli aliboa sana. Hata maadili ya kawaida tu hana. Pengine ni utoto.
ReplyDeleteMimi ninamuunga mkono Mh. Mbunge, kwani waTZ mmekuwa limbukenii na kiingereza mno mpaka inatia kichefuchefu.
ReplyDeleteIcho kingereza wanakiabudu kama mungu vile na sio kwamba hajui kiswahili bali ana mashauzi ya panya kujipitisha mbele ya wageni
ReplyDelete