Stori: Denis Mtima na Chande Abdalla
MTOTO Kulendya Rojason (3) ambaye siku za nyuma aliwahi kuripotiwa na vyombo vya habari kuwahi kulelewa na mbwa baada ya wazazi wake kumtelekeza yeye na ndugu zake, bado anazidi kuteseka kwa kukosa msaada wa chakula
Akizungumza kwa niaba ya mtoto huyo nyumbani kwao, Nyerere B, Mabatini Mwanza, dada wa mtoto huyo, Recho Rojason (18) alisema kuwa mdogo wake bado anateseka kwani hapati malezi ya kutosha kutokana na maisha yao kuwa magumu.
Recho alisema kuwa, maisha yao yamekuwa magumu baada ya mama yake kuwatelekeza na kuolewa na mwanaume mwingine huku akimwacha baba yao ambaye ametopea kwenye ulevi na kushindwa kutoa msaada wowote.
Recho ambaye ni hausigeli anayefanya kazi kwa ujira mdogo maeneo ya Mwanza Mjini, alisema wamekuwa wakipata fedha kidogo kutoka Halmashauri ya Jiji ambapo hazikidhi mahitaji yao na kuwaomba watu wajitokeze kuwasaidia.
Aliomba msaada wa kupata fedha kwa ajili ya matibabu, masomo na malazi kwa kuwa yote hayo ni mahitaji yao yeye pamoja na wadogo zake watano akiwemo Kulendya.
Akizungumzia sakata hilo jirani anayeishi na watoto hao, Chausiku Ibra alisema kuwa watoto wa familia hiyo wamegeuka machokoraa kutokana na huduma hafifu na kuongeza kuwa mtoto wa mwisho (Kulendya) ndiye yupo hatarini zaidi.
“Huyu mtoto wa mwisho ndiye aliye hatarini zaidi kwa kuwa tangu alivyokuwa mtoto alikuwa akiletewa chakula na kutunzwa na mbwa.
Mpaka anakuwa hivi ni jambo la kumshukuru Mungu kwa kweli. Watoto hawa wanahitaji msaada jamani,” alisema jirani huyo.
Waandishi wetu walijionea, nyumba wanayoishi watoto hao ambayo imeonekana kuharibika kwa kiasi kikubwa sehemu za paa na kuta jambo ambalo ni hatari kwa watoto hao huku taarifa zikieleza kuwa, baba wa watoto hao, Rojason Ernest amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando akiuguza nyonga baada ya kuanguka akiwa anatokea kilabuni.
Kama umeguswa na unataka kuwasaidia watoto hao, wasiliana nao kwa namba ya jirani yao, Chausiku: 0767445683.
Imeandikwa na Global Publishers
Mpekuzi Acha Usenge, Rudisha Coment Yangu Kiroho Safi! Au Sababu Nimemtaja Kapuya?
ReplyDeleteHahahahahagpahaha kama harudish inakuwaje
Deleteduh! poleni mungu atawasaidia watoto
ReplyDeletewacheni uongo mnataka hela za bure tu! hakuna mtoto anaeweza kulelewa na mbwa hata siku moja!
ReplyDeleteWatanzania wamegundua njia mpya za kuomba omba hela kama Rais wao….
ReplyDeletekanusha kauli yako shwain rais si mtu wa kutukanwa kama wewe hovyohovyo
DeleteMh
ReplyDelete