"MGOGORO ULIOPO NDANI YA CHADEMA NI KAZI YA MAKACHERO..." DR SLAA AFUNGUKA

KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa amesema mgogoro uliopo ndani ya chama ni kazi ya makachero. Alitoa kauli hiyo jana jioni alipokuwa akihutubia mamia ya wananchi wa Mji wa Kahama mara baada ya kuwasili akitokea jijini Dar es Salaam akiwa njia kuelekea mkoani Kigoma kwa ziara ya wiki moja.
  

Dk. Slaa ambaye alifika saa 12 jioni alitumia muda dakika zisizozidi 20 kuhutubia ambapo alisema chama hicho kina taarifa za ushiriki wa makachero, lengo likiwa kukidhoofisha na hatimaye kukisambaratisha chama hicho.

“Tunazo tayari taarifa kuwa makachero ndio wapo nyuma ya mgogoro ndani ya chama, wameingia kwa nia ya kutuvuruga, lakini tupo imara.

“Nawasihi Watanzania waache kushabikia vitu visivyo vya msingi, badala watumie muda wao kufikiri na kufanya mambo ya msingi kwa Taifa.

“Yote yanayotokea katika chama chetu kwa sasa yanatuandaa na kutukomaza kwa ajiri ya kuchukua madaraka ya nchi mwaka 2015,” alisema.

Alisema kuwa, wanachama wote wa Chadema wanapaswa kujua hakuna aliye juu ya Katiba ya chama hicho, kwa hiyo Katiba italindwa na kusimamiwa bila woga kwa maslahi mapana ya chama.

Leo anatarajiwa kuondoka na msafara wake kuelekea mkoani Kigoma, ambako kituo chake cha kwanza kitakuwa eneo la Kakonko na baadae ataelekea Muhambwe.

Katika ziara hiyo ya kukagua uhai wa chama atatembelea mikoa ya Shinyanga, Kigoma, Tabora na Singida.
-Mtanzania
Tags

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. wachaga mmeanza kusingizia makachero ehhhn!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  2. Acha umbulula we anony hapo juu, kakwambia nani dk slaa mchaga? Usishabikie vitu ambavyo huna uhakika navyo.

    ReplyDelete
  3. Bac wa kaskazn kuma we.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hv kwann watanzania tuna ubaguzi sana?afu tukibaguliwa na mataifa mengine tunalalamika.mara ukabila, mara udini, ukanda, albino, nadhani kinachofuata sasa hv ni kuwabagua wenye vipara, wafupi....ila yote ni kukosa shule

      Delete
  4. Mbowe we na elimu yako form six unataka uongoz c anaendeshwa na bangi huyu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mbona form six kubwa...Kagame ni kiongozi wa Rwanda elimu yake ni form two, lakin kafanya mambo makubwa sana kwa nchi yake kwa kipind kifupi

      Delete
  5. Oya Aachen matuxi!!!

    ReplyDelete
  6. SLAA NOMAA ACHENI HAYO MAMBO

    ReplyDelete
  7. Huyo Zito mnae mtetea aanzishe chama chake kama anafikiri kuwa ana ushawishi mkubwa kuliko wanasiasa wote. Huko atapata wafuasi na atakuwa mwenyekiti kama ndiyo shida yake.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad