Kama nilivyo elezea kwenye kichwa cha habari hapo juu,
siku hizi watu wengi wamekuwa na mtindo wa kuajiri wasichana wa kazi (mahouse girl) ili kusaidia kazi za nyumbani.
Ndio hatukatai pengine mama mwenye nyumba anaweza kuwa anazidiwa na kazi,
Kama kufua nguo za mzee,watoto,kunyoosha, kuandaa chakula nk.
Lakini kuna wadada/wanawake wengine unakuta watu wako wawili yeye na mumewe,
eti nao wanaweka house girl sijui wa nini?eeh!!!
tena wengine sijui ni sifa eti anaajiri wawili kabisa kwa kazi zipi sasa?na wewe ufanye kazi gani?
Ya kupaka rangi kucha na kuchat kwenye mitandao? halafu bila aibu unasifia chakula alichoandaa house girl mbele ya mumeo.
Na unaangalia tu house girl anamnawisha mikono mumeo na kumkausha na taulo,wewe upo tu kwenye kiti kama umegundishwa na super glue vile.
huyo jamaa yako akila chakula kitamu cha house girl, si atataka ale na kile cha usiku aone utam wake?
hapo ndipo timing zinapoanzia na ukizingatia mahouse girl walivyo na heshima,
baba akifika na kamzigo anapokelewa kwa mikono miwili na anapigiwa goti,
wakati huo we upo upo tu kama koti la mvua linasubiri masika.
Sijui ndio kusema hamuelewi mko pale kwa ajiri gani?na house girl akiboronga kidogo tu macho na sauti ya ukali inakutoka kama nini,
Hujui kwamba unapofanya hivyo unamkomaza house girl,hapo kwako ni sawa na chuoni kwake anachukua mafunzo ya maisha.
Mumeo akisifiwa kazini nguo zake zinang'aa atamkumbuka house girl,
akisifiwa kwamba ananawili atamkumbuka house girl,
akisifiwa kwamba viatu vyake vinang'aa atamkumbuka house girl,
Ndio si house girl ndio anaye fanikisha yote hayo?wakati wewe uko bizy ku up load picha fb?
mwisho wa siku unatemwa kama big G iliyo chacha,
halafu watu wanabaki kushangaa mbona jamaa kamuacha mwanamke mzuri vile halafu kabeba house girl?
kumbe ni janga la kitaifa hajui A wala B kifupi hajitambui,
Badilikeni nyie kina Eva ma house girl watawapiga bao ohooo!!!!!!
acha mfumo dume kaka ndio maana huna mke mpaka leo, umeoa mke msaidiane kazi sio akufanyie kazi na wewe baba kazi yako nini? huwezi kufua nguo? huwezi kujinawisha mikono? unaulemavu gani mpaka kila kitu ufanyiwe na mkeo? ndio nyinyi mnaoa watumwa badala ya mke acha mawazo mngando ndoa itakushinda
ReplyDeletewewe naoda limekuchoma mpaka ktkt ya moyo na bla shaka unahusika hizi tabia,badilka haraka sana maana huwezi kubadilisha dunia kwa masaa 24,mwanaume ndivyo alivyoumba so kama unaweza kuitoa tabia aliyoiweka mungu katk mwili wa mwanaume toa...
Deletesasa ulichelewa wapi? kwani housegirl sio mwanamke wewe vipi?
ReplyDeleteAnataka Kila kitu afanyiwe yeye kiwete.hata mlambwe mikono kwa kuoshwa kama jitu linatabia chafu huwezi kubadili.
ReplyDeleteadmin hao wanaocoment upuzi achana nao umenena sana maana inafikia kipindi ht kutomban.... wamama wa nyumbani hawawezi lkn housegirl cmchezo
ReplyDeletehaus gelo ukishamuoa tu na yeye atataka msaidizi wa ndani, yaani fikra zao huwa zinabadilika utatafuta sana tu kila haus gelo akisha vishwa pete na yeye anataka kula bia na wewe sitingi ruum
ReplyDeleteHivi kwanini watu wanakuwa na akili mgando sana?? Mwanaume anapewa ukingo wa kufanya malaya kisa mkewe siyo kijakazi wake??? Woote wanafanya kazi, woote wanaleta hela mezani, huyo mama amzalie na kumtunzia watoto, libaba limekalisha mkundu chini tu. Afanye na yeye kazi, ndoa ni kusaidiana siyo utumwa, siku mmkibadilisha akili migando mliyolelewa katika familia zenu dunia itakuwa na madiliko mazuri sana.
ReplyDeletehivi kazi ya mwanaume ni nini haswa? unajua malezi ya kumpakata mwanaume mpaka anakuwa bogus na kumpelekesha mwanamke kama kijakazi yamepitwa na wakati! badilikeni basi ni aibu mpaka millenia hii tuna wanaume/wanawake mabogus wanaofikiria wanawake wako kwaajili ya kuwaservice wanaume tu, na hao wanaume wana waservice waakina nani?mama zao?
ReplyDeleteUpuuz mtup
ReplyDeleteMajanga
ReplyDeleteSiwezi kugeuka kuwa mtumwa wa mwanaume eti kisa nisiachike. Nitafanya kazi pale ninapoweza tu siwezi kujichosha bure kuogopa kuachika. Mijanaume yenyewe mi macho kodo kodo hata ujipinde na mikazi yoote bado jitu liacheat huko nje Kama sio house girl au baby sitter yaani ni mijanga na uvurugaji tu. Tena mijitu Kama hii ni kuiua haina maana kugeuza wake zao vijakazi mtawapata wajinga hai hao
ReplyDeleteHii habari sio kweli.mwanaume kulala na house girl ni ufirauni wake tu, haina uhisiano sijui anakuletea chakula, ooh mara maji ya kuoga nk.Mbona watu wengine wanaacha wanawake wao wazuri nyumban afu wanaenda kununua Malaya? ni tabia za mtu kwa namna alivyolelewa
ReplyDeleteMimi jamani namtamani sana housegirl wangu ni msafi,anapika vizuri na kwa wakati,ni ka-model,mtii,beautiful,nk.nk.Mke wangu anazidi kunenepeana,kukoroma usiku kucha,mbishi,hanijali,hana kazi lakini haingii kabisa jikoni,nifanya je hapa wajameni?
ReplyDeletehouse girl wazuri wanaheshima, na heshima yao haichuji kwa kuwa wako kwenye mafunzo shida ni mama na baba kutoweza kumlelea km walimu wake au kusimama km mzazi,pia hizi tabia zipo mashariki ya kati,na afrika ,ulaya haya mambo hakuna ,kila mtu anajua kazi yake km umefika nyumbani unapika ,hakuna cha kusubiri mke,ila bado kunawaliokuja na tabia zao za huko ,hawajabadilika ,unapika chakula chako na watoto wako sijui km ,hapa ni kuolewa ,au kuoa ni kupikiwa tu? etc
ReplyDelete