MWANAMUZIKI FM ACADEMIA AFANYIWA KITU MBAYA

Na Shakoor Jongo
DUNIA kweli haina huruma! Kitendo alichofanyiwa  mwanamuziki wa Bendi ya FM Academia ya jijini Dar  anayejulikana kwa jina moja la Flora alfajiri ya kuamkia Desemba 8, mwaka huu ni kibaya katika jamii ya Kitanzania.
Flora akiwa amepata kinywaji ili kuchangamsha mwili wake alijikuta akipigwa na vijana wawili wanaofanya kazi ya kuendesha Bajaj akiwa amewakodi kwa ajili ya kurudi nyumbani  kwake.
Wananchi wakipanga jinsi ya kumsaidia Flora.
Tukio  hilo lilitokea maeneo ya Mwananyamala jirani na MK Pub jijini jirani kabisa na ofisi ya Msanii Tuesday Kihangala ‘Mr Chuz’ limeacha simanzi kubwa kwa wakazi wa eneo hilo.
Mmoja wa wananchi akijaribu kumnyanyua Flora.
Kwa mujibu wa shuhuda wetu inadaiwa kuwa, Flora alipigwa na vijana hao na kuporwa  vitu vyake vya thamani ikiwemo simu pamoja na pochi lililokuwa na kiasi cha fedha ambavyo vyote bado havijajulikana  thamani yake.
...Akiwa hoi.
Mbali na kumpiga,  vijana hao waliokuwa waliokuwa wakisaidiana kufanya kazi katika Bajaji hiyo wanadaiwa kumvua nguo mwanamuziki huyo ambaye aliwahi kutunga na kuimba kibao cha Sintasahau huku akishiriki kuimba vibao vingine vya FM Academia kama vile Dunia Kigeugeu, Shida  na Heshima kwa Wanawake.
...Akijiegemeza kwenye gari.
“Tulikuwa tumekaa naye hapa tukila chips (MK) baada ya kumaliza kula Flora alionekana akikodi Bajaj ili kurudi  nyumbani kwake, baada ya muda tukawaona watu wakikimbilia kule kwenye ofisi ya Chuz, tulipoenda tukamkuta Flora akipewa msaada na mlinzi  na mwanamuziki mwingine kutokana na unyama aliofanyiwa,” alisema shuhuda  huyo.
...Akivishwa nguo.
Naye mlinzi aliyekutwa eneo la tukio alipoulizwa kuhusina jinsi kitendo hicho kilivyotokea, alisema kuwa aliiona Bajaj ikisimama eneo hilo na watu wanne wakashuka akiwemo Flora na baada ya muda kidogo alimuona mtu akijikokota alipomsogelea ndipo alipomuona  mwanamuziki huyo akiwa amevuliwa nguo.
...Baada ya kuvalishwa nguo akawa anasaidiwa na wasamaria wema.
“Wamemfanyia unyama sana wale vijana, sijui nini kingetokea kama ningegundua kabla hawajatenda unyama wao,” alisema mlinzi huyo aliyekataa kutajwa jina lake gazetini.
Flora aliondolewa eneo hilo baada ya kupewa msaada wa nguo na mmoja wa majirani wa eneo hilo ili ajisitiri.
Baada  ya tukio hilo, mwandishi wetu alimpigia simu Kiongozi wa FM Academia, Nyoshi El Sadaat lakini hakuweza kupokea ndipo akahamia kwa mwanamuziki wa bendi hiyo, Patcho Mwamba na kumuuliza kama Flora bado yuko FM Academia.
...Akipelekwa sehemu salama.
Patcho alikiri uwepo wa Flora katika bendi yao lakini alisema kwamba siku hizi mbilI hajaonekana na alisikitika alipopewa kisanga hicho kilichomkuta.
“Ni kweli tunaye Flora lakini siku hizi mbili hakuwepo kazini dah! Wamemfanyia unyama sana, madereva  wengine wa Bajaj si watu wazuri,“ alisema Patcho.
Mpaka sasa haijajulikana kama Flora alitoa taarifa za tukio hilo polisi au la, jitihada za kumtafuta zinaendelea.
GPL

Post a Comment

10 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Very sad!! I hope awo wanyama watakamatwa nakuchukuliwa hatua za kisheria! Ivi unawezaje kumfanyia binaadam mwenzio unyama kama huo!?

    ReplyDelete
  2. Kwani amewaambia yeye hana uwezo wa kununua hilo li suruali lenu au aliamua makusudi kuvaa vile. Mwacheni avae uchi bhana aone faida zake!

    ReplyDelete
  3. we anoy no 2 ni mkundu kweli sasa hapo ndo umeongea pumba gn.. mijitu mingine bana kama inasuguliwa gaga.. pole dada flora

    ReplyDelete
  4. te te sina mbavu mwenzenu mtaniua

    ReplyDelete
  5. te te sina mbavu mwenzenu mtaniua

    ReplyDelete
  6. KPND ANA PGWA HAKUPIGA HATA KELELE? HUYO MLNZ AKAMSAIDIA? MH!HAWA NDO BNADAM WA ADAM

    ReplyDelete
  7. such people are just worthless and they are supposed 2 be burnt to death, i hate such men.they are the people who can rape there mothers...........fooooooooooooooooooools..... NKT.

    ReplyDelete
  8. You better comment in swahil if english is your mother in law!!

    ReplyDelete
  9. hii midereva bajaji ilizaliwa mikunduni si haba tena na wakigyndulika ikafirwe na mibaba 120 mpaka washonwe bomba wakaafilie misituni hawastahili kuitwa binadamu fyuuuuuu

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad