Msanii mkongwe wa vichekesho Said Ngamba almaarufu kama Mzee Small, amemlaani mtu aliyetoa taarifa za uongo kuwa amefariki dunia jana usiku.
Akizungumza na tovuti ya Bongo5 waliomtembelea nyumbani kwake Tabata Mawenzi leo asubuhi, Small amesema alipatwa na mshituko baada ya kupata taarifa kuwa kuna watu wanasambaza taarifa kuwa amefariki dunia, na kumlaani mtu aliyosambaza taarifa hizo za uongo.
“Kwanza nawashukuru (Watanzania) na nawaheshimu kunipigia simu na kumtafuta mchawi, maana yake nyinyi ndiyo mumemvumbua mchawi,nawashukuru Radio zote,Tv zote nazishukuru mimi mzima bado nipo hai” Alisema Mzee huyo mcheshi.
“Kwanza mke wangu alishituka alafu mimi mwenyewe nilikuwa nimelala, lakini kwakweli mimi nilijisikia vibaya, namalaani huyo mtu,namlaani kwanzia leo mpaka kiama na mwenyezi mungu atamuona na kumsikia” Alisema Mzee Small.
Naye mke wa Mzee Small amesema kwa upande wake ameathirika kwa kiasi fulani kwakuwa yeye ni muuguzi mkuu, alihitaji kuulizwa maendeleo ya Mzee Small kabla ya kutangaza taarifa za uongo.
“Mimi ni mke wa Mzee Small kwakweli kwa tukio lililotokea limeniumiza sana kwasababu mimi ndiyo muuguzaji mkuu wa huyu bwana,niko nae inakuwa vigumu jambo kama hili linapotokea wakati mimi sijui chochote, kwakweli limeniumiza. Nawaomba Watanzania tufike mahala tuangalie, tusianze kusambaza vitu ambavyo hatuka ukweli navyo” Alisema mke wa Small.
laanatullah kwao washamba na wanafiki hao na utaishi miaka 800 pamoja xana jembe
ReplyDeleteWalaaniwe kabisa! Tunakutakia maisha marefu yenye afya tele mzee wetu.
ReplyDeletendo tatizo za media za bongo, kusambaza habari kabla hawajajua ukweli
ReplyDeletemmfyuuu jitu lililozusho halina hata habari si ajabu linagida mibia likijisifu. shenzy zenu mnaizushia wenzetu vifo mtatangulia nyie Mungu hapangiwi wakumchukuwa.
ReplyDeletesio changudoa lulu ndo kaweka picha yako na kusema r.i.p kuma mamako wewe weumemuua kanumba na ndo unataka kumuua babu ye2 malaya we?
ReplyDelete