Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye ameeleza kupokea kwa faraja, hatua ya mawaziri wanne kuenguliwa nyadhifa zao kwa ridhaa ya Rais Jakaya Kikwete.
Mawaziri hao, Khamis Kagasheki wa Maliasili na Utalii, Dk Emmanuel Nchimbi (Mambo ya Ndani), Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamshi Vuai Nahodha na Waziri wa Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi, Dk Mathayo David Mathayo walijiuzulu nyadhifa zao baada ya wizara zao kuelezwa kushindwa kusimamia Operesheni Tokomeza Ujangili, ambayo ripoti yake iliwasilishwa bungeni juzi na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, James Lembeli.
“Najisikia vizuri, maana kwa kitendo cha mawaziri hao wanne kuchukuliwa hatua, ninaamini kitasaidia wale wengine waliolala nao waamke. Bila shaka sasa hakuna atakayelala na akilala anajua itakula kwake,” alisema Nape alipokuwa akizungumza na Kituo cha Televisheni cha ITV cha jijini Dar es Salaam alipotakiwa kueleza hisia zake kwa uamuzi huo wa Bunge.
Wakati Waziri Kagasheki akiwa ametangaza mwenyewe hatua ya kujiuzulu wadhifa wake, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alitangaza hatua ya Rais Jakaya Kikwete kubatilisha uteuzi wa mawaziri hao baada ya wabunge kushinikiza wajiuzulu kutokana na Kamati ya Kudumu ya Ardhi, Maliasili na Mazingira kubaini ‘uozo’ katika Operesheni Tokomeza Ujangili iliyofanyika hivi karibuni.
Chini ya Mwenyekiti wake, James Lembeli, Kamati hiyo ilieleza pamoja na mambo kadhaa iliyoyaeleza kuwa ya ovyo yaliyojitokeza kwenye operesheni hiyo, vitendo vingi ikiwemo ubakaji na udhalilishaji vilifanyika ambapo ni kinyume na utu na haki za binadamu.
Kutokana na kadhia hiyo, kamati hiyo kupitia kwa Lembeli, iliwataka mawaziri wanaohusika kutazama kama wanafaa kuendelea na nyadhifa zao au wajiuzulu, pia kamati hiyo ikaenda mbali zaidi kwa kumwomba Rais Jakaya Kikwete kuchukua hatua ya kuwawajibisha.
Akizungumzia zaidi hatua hiyo, Nape alisema kuwa pamoja na mawaziri hao kuwajibika, ipo haja ya kwenda mbali zaidi kwa kutazama mifumo na sheria zilizopo sasa kwa kuwa inaonekana kuwa miongoni mwa vyanzo vya vikwazo katika utekelezaji wa utawala bora.
“Kwa mfano leo hii, mawaziri wameng’oka, sawa ni jambo jema, sitetei, lakini inawezekana kabisa kuna mifumo na sheria ambazo zilimkwaza waziri huyu kutimiza wajibu wake. Mfano, alihitaji kumfukuza mtu kazi kwa kuzembea jambo fulani, lakini mamlaka ya kufukuza kazi mtumishi yapo kwa Katibu Mkuu wa Wizara, hapa atafanyaje,” alisema Nape na kuongeza;
“La msingi hapa ni lazima hatua hizi ziende mpaka chini huku kwa watendaji, ili isiwe mawaziri wanawajibishwa tu kwa sababu ya dhamana zao za kusimamia kisiasa, huku watendaji wanazidi kuvuta shuka bila hofu wakati baadhi yao ni sehemu ya matatizo”.
Alisema kuwa hatua ya sasa inayofanywa na CCM kusimamia Serikali ni ya kawaida kwa kuwa kazi hiyo haipaswi kufanywa na wapinzani kwa kuwa sera inayotekelezwa ni ya chama hicho.
Nape aliahidi CCM kukomba viti vyote vya ubunge na udiwani vilivyopo chini ya wapinzani, akisema, baada ya wapinzani kujaribiwa wameshindwa kuonyesha matunda yoyote ya kusaidia wananchi na hivyo kutokuwa mbadala wa CCM
Tunapokuwa na wanasiasa wa aina ya Nape katika nchi yetu ndiyo maana tutabaki kula vumbi tunalotibuliwa na majirani zetu
ReplyDeleteMbona Hawa Ghasia wamemuacha?Rais mwenyewe anassingizia ugonjwa wakati nchi ipo kwenye crisis.
ReplyDeleteMBONA PINDA HAWAJAMTOA?
ReplyDeletehivi kujiudhuru 2 au kufukuzwa inatosha wakati watu wamefirwa na wengine kufa! na ujangili unaendelea kufanya tena kwa kiwango kibubwa na madalari ni hao hao serkalin?
ReplyDeleteHao walioachishwa tusije kesho tukawasikia ni mabalozi!Tanzania hii wenyewe wanajuana siri zao,
ReplyDeletekwa kumwita nape mwanasiasa ni kumpandisha cheo, yeye ni mpiga domo tu pale
ReplyDeleteSINA UHAKIKA MWENYEKITI WAKO ANAKUBALIANA NA KAULI YAKO
ReplyDelete