DUNIA yamlilia Nelson Mandela, ndivyo inavyoweza kuelezwa kwa maneno machache kuelezea namna msiba wa shujaa huyo wa vita dhidi ya ubaguzi wa rangi ulivyogusa mioyo ya watu wa rika, rangi na mataifa mbalimbali duniani.
Kifo cha Mandela, maarufu miongoni mwa raia wenzake wa Afrika Kusini kwa jina la Madiba kimethibitisha pasi na shaka kwamba, ameondoka mwanadamu maarufu zaidi duniani ambaye alama alizoacha nyuma yake zinampambanua kuwa mtu asiyeweza kulinganishwa na mwingine yeyote.
Kwa Watanzania, machungu ya kifo cha Mandela kilichotokea juzi usiku yanaweza yakalinganishwa na yale ya Oktoba 14 mwaka 1999, wakati taifa lilipompoteza Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere.
Si ajabu hata kidogo kwamba, mwangwi wa msiba huu wa Madiba, kipenzi kikubwa kwa watu wa rangi na asili tofauti nchini mwake, umesafiri na kufika katika kona zote za dunia kwa kiwango cha kuwaliza watu maarufu zaidi hadi wale wa kawaida.
Ni kutokana na uzito wa msiba huo, ndiyo maana serikali ya Tanzania jana ilitangaza siku tatu za maombolezo ambazo zinakwenda sambamba na kupepea kwa bendera nusu mlingoti.
Hali kama hiyo ndiyo pia iliyoonekana hata nchini Marekani ambako taifa hilo kubwa kabisa duniani limeingia msibani kwa namna inayoonyesha kwamba aliyefariki dunia alikuwa raia nambari moja wa dunia.
Ni kwa kulitambua hilo na kwa kujua ukweli kwamba Mandela hakuwa tu mali ya raia wa Afrika Kusini ndiyo maana taarifa rasmi ya kifo hicho iliyotolewa na Rais Jacob Zuma ilikuwa na maneno yenye ujumbe wenye maneno mazito.
"Taifa letu limempoteza mtoto wake mkuu wa kiume. Watu wetu wamempoteza baba. Licha ya kwamba tulifahamu kuwa siku kama hii ingemtokea, hakuna kinachopunguza upendo wetu kwake na hasara kubwa tuliyopata. Jitihada zake kutafuta uhuru zimemjengea heshima kubwa duniani.
"Unyenyekevu wake, upendo wake na utu wake, vimesababisha watu kumpenda. Mawazo yetu na sala zetu tunazielekeza kwa familia ya Mandela. Kwao tuna deni kubwa la kuwashukuru. Walijitolea kwa kiasi kikubwa na kuvumilia mengi ili watu wetu wawe huru,” alieleza Zuma wakati akitangaza kwa mara ya kwanza msiba huo mzito.
Hakuishia hapo, Zuma aliwataka watu wanaomlilia Madiba duniani kote kukumbuka mambo ambayo Madiba alipigania.
"Hebu tujibidishe bila kupoteza nguvu kujenga Afrika Kusini yenye umoja, isiyo na ubaguzi wa rangi, isiyo na ubaguzi wa kijinsia, Afrika Kusini ya kidemokrasia na ustawi. Hebu tueleze kwa namna yetu wenyewe, shukrani kubwa tuliyonayo kwa mtu ambaye ametumia muda mwingi kuwatumikia watu wa nchi hii na kwa minajili ya utu,” alisema Zuma kwa uchungu.
Nyerere is my first president period
ReplyDeleteWe nawe? kwani umelazimishwa kumpenda Mandela? Hovyooooo
ReplyDeletebwegee kwel huyo
ReplyDeleteMandela ndiye mtu pekee chini ya jua aliyekuwa hana adui,anaombolezwa hadi na mahasimu kama marekani na syria kila kona ya dunia toka japan hadi paraguay, toka holland hadi new zealand.Ahaaaa Tata Madiba no one like you for sure
ReplyDeleteSio kweli?mbona hakumsamehe mke wake Winnie!alilofanya mandela kubwa ni kuwasamehe waliomtendea mabaya.Lipi lingine alilowafanyia wana SA?kama ni ukombozi kuna watu walifanya juhudi sio mandela
Deletehilo nalo neno aliwezaje kuwasamehe makaburu walioua watu kibao but mkewe hakumsamehe katu, mh huwezi jua siri kubwa bas ukiona hivyo hata mungu hataweza kumsamehe pia, but mandela ni mfano wa kuigwa
ReplyDelete