PESA ZA WATEJA WA M-PESA, TIGO PESA, AIRTEL MONEY NA Z-PESA WANAO FARIKI ZINAKWENDA WAPI?

Kutokana na makampuni karibu yt ya simu Tz kuwa na huduma hz za mobile money, Je inapotokea mteja amefariki, makampuni yanawajibika vipi kuhusu kurudisha pesa za mteja wao kwa msimamizi wa mirathi au warithi? 

swali hiili linazingatia kuwa wateja wanaoweza kutwa na mauti kwa vyovyote wanaweza kuwa na akiba kidogo kwenye ac zao za mitandao ya simu wanayotumia!

Je kuna sheria yoyote ambayo imeweka bayana masuala haya?

kwa wenzetu walio kwenye makampuni ya simu tafadhali mtusaidie kwa hili!
naomba kuwasilisha kwa mjadala!

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. hapo kweli utata,inabd watueleze vzur.

    ReplyDelete
  2. Aisee, hapo nadhani na pesa ndo zinakufa

    ReplyDelete
  3. Mdau uliwakilisha mjadala huu pongezi sana. Ni muhim sana vyombo vya sheria, wanaharati na hata bunge la nchi kulitupia macho kwa karibu. Makampuni yote ya sim yanayotoa huduma ya m-pesa yatoe maelezo (TERM & CONDITION) ni hava gani za kufuata ikiwa matatizo yaliyolezwa hapo juu yatatokea.

    ReplyDelete
  4. Cha msingi watu wawe wazi kwa wenye ndoa waambiane password za line zao ie TIGO,VODA,AIRTEL MONEY ili hata ikitokea chochote mmojawapo anaweza kwenda kutoa pesa iliyopo.Kwa wasio na ndoa wachague watu wanaowaamini kama wazazi wao wawekane wazi kwa hili tatizo, watu wamekuwa wasiri mtu ana Acount benk hata mkewe haijui so ikitoke mtu akatangulia mbele za haki waliopo watakosa pa kuanzia.

    ReplyDelete
  5. siku mbili admin unaongea vitu vya maana sana, keep it up.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad