RAY C AANIKA VIGEZO VYA MUMEWE MTARAJIWA

Na Gladness Mallya
STAA wa muziki wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’ ameibuka na kusema kuwa anahitaji mume anayemzidi umri kwa miaka kumi.

Akizungumza hivi karibuni kwenye kituo kimoja maarufu cha runinga, Ray C alisema anahitaji mwanaume mtu mzima anayemzidi miaka kumi, anayejitambua na asiwe mwanamuziki kwani anaamini akiwa na mtu kama huyo uhusiano wao utakuwa mzuri kuliko ule wa awali uliokuwa wa machungu.

“Ninamtaka mwanaume anayenizidi miaka kumi kwani kwa sasa nina miaka 31 japokuwa kwa sasa nafanya kazi kwanza ili nirudi kwenye levo yangu na nitakuwa juu zaidi ya zamani kwa sababu najitambua japokuwa nina hamu sana ya mtoto lakini yote namwachia Mungu.

“Nashukuru sasa hivi niko vizuri nakumbuka  meneja wangu wa kwanza alinikataza nisiwe na uhusiano na mwanamuziki lakini ndiyo hivyo nikajikuta niko na Lord Eyes ambaye alianza kunichanganyia cha Arusha (bangi) bila mimi kujua na kujikuta ninaharibikiwa lakini nimeshamsamehe na ninamuombea heri katika maisha yake,” alisema Ray C.

Aidha, Ray C alisema anamshukuru Mungu kwa sababu hana mume wala mtoto kwa sababu kwa jinsi alivyokuwa mwanzo angejenga picha mbaya sana kwa mwanaye.

“Wakati nilipokuwa na matatizo nilijifunza mengi kwamba hakuna rafiki wa kweli kwa sababu walinipenda nikiwa mzima lakini nilipokuwa naumwa hakuna hata mmoja aliyenipigia simu kunijulia hali zaidi ya mashabiki zangu tu kwa hiyo nimebadilisha mfumo wa maisha yangu,” alisema Ray C.

Miezi kadhaa iliyopita, mwanamuziki huyo alitangaza kuachana na madawa ya kulevya ambayo alikiri kuwa yalimharibia mwenendo mzima wa maisha yake.

Post a Comment

15 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. we ray c umeshaisha kila siku unatafuta kiki na mastory ya ajabu ajabu.. atakaetaka kukuoa nani teja mkubwa ww.. ona ulivyojiharibu na mkorogo umekua kama nguruwe

    ReplyDelete
  2. kurudi kwenye revo yako sahau dada labda utafute huyo mwanaume mtu mzima akuoe na kupata mtoto kama kweli unahamu na mtoto. utulie tatizo sembe bado inaongea kichwani tutakuaminije

    ReplyDelete
  3. mteja tu huyo muacha akale unga wake huko asizimgue watu!

    ReplyDelete
  4. We bibi sasa utulie, mshukuru JK umepata nafuu, ila bado hujapona. unatia aibu, kubwa Zima kila siku na mistory ya kijinga huoni aibu, hivi hujui wakati wako umeshapita? unadhani sasa hivi na wewe unaweza kushindana na akina wema. Lione kwanza, nene linanuka jasho tu na kikwapa, nenda kale unga huko.

    ReplyDelete
  5. Ule wakt uliouchezea haujag mara mbil mama ht iweje...mda wako ushaisha acha kulazimisha mambo....tulia.ishi km vile hujawah kuwa star utaona maisha yatakavyokuwa rahis na utayafurahi...unayotafta ss iv ni kujitia aibu tu hamna lingine

    ReplyDelete
  6. Ule wakt uliouchezea haujag mara mbil mama ht iweje...mda wako ushaisha acha kulazimisha mambo....tulia.ishi km vile hujawah kuwa star utaona maisha yatakavyokuwa rahis na utayafurahi...unayotafta ss iv ni kujitia aibu tu hamna lingine

    ReplyDelete
  7. Ahsanteni wadau...mmempa makavu live...

    ReplyDelete
  8. Nyie hapo juu wote ndo mateja na wasenge wakubwa,hakuna linaloshibdikana chini ya hili jua leo hii rayc kafanikiwa watu wote mtaanza kumsifia sawa na lulu alivyowekwa ndani kila mtu alimponda leo hii kila mtu anamsifia oh lulu mzuri oh lulu ana kipaji,watanzania hawana jema!

    ReplyDelete
    Replies
    1. acha ufala wewe au nawewe unavuta nae????????????????????????????????

      Delete
  9. achana nao hao wote we mkabidhi mungu maisha yako na utafaanikiwa sawa mdada cz hakuna binadamu asiyekosea ila jifunze usirudie kosa

    ReplyDelete
  10. Dia dada hayo ni maneno tu hata kwa kanga yapo so so do wat u wat to do acha na ya watu hayana faida peta dada yangu yaingie kushoto yatoke kulia dada all de best

    ReplyDelete
  11. wote wanaokuponda nikwa sababu hayajawafika lakini siku yakiwapata watatia akili. fuck all of you who make her 2 regret what she did with her life, but i think she is better than some of you .

    ReplyDelete
  12. HANA LOLOTE HUYO,KUNA MZEE MMOJA MAARUFU SANA HUKO JIJINI ARUSHA NDO ANAMLEA KWA SASA,HUYO MZEE NI BOSI MKUBWA SANA KWENYE MOJA YAPO YA KAMPUNI KUBWA YA MIKOPO HAPA TANZANIA! KAMA ANABISHA NIMTAJE HAP HADHARANI!

    ReplyDelete
  13. jameni kwani ni vibaya mtu kusema vigezo vya bwana ampendaye? mmmhh shakuwa tabu....lol!!!!

    ReplyDelete
  14. huyu teja vp????????????????silipendi mimacho kama vile kakurupuka kutoka JEHANAM

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad