SABABU ZA KWANINI HOTUBA YA JAKAYA KIKWETE KUMUAGA MANDELA ILIKUWA BORA ZAIDI

Ndugu zangu, 

NOTHING can come from NOTHING. Wamesema hili Wanafalsafa wa Uyunani ya Kale .

Nimemwona na kumsikiliza Rais wetu Jakaya Kikwete akizungumza kwenye siku muhimu ya kumuaga kwa mara ya mwisho Mzee wetu Nelson Mandela. 

Muda wote wa hotuba yake, JK alibaki kwenye mstari kwa namna ile ile ya kuweka bayana kwa ulimwengu, kuwa ' msione vinaelea'. 

Hakika alichofanya JK leo ndicho haswa alipaswa kukifanya, na amekifanya kwa kutumia weledi wake kwenye diplomasia na kuchanganya uzoefu wake kwenye uongozi wa kisiasa na dola kwa ujumla.

Ni kuitumia fursa ile ambapo macho na masikio ya dunia yalielekezwa Quni, kwa yeye rais kuiambia dunia, na si kuisubiri CNN au vyombo vya habari vya Kimagharibi kuifanya kazi hiyo, juu ya mchango wa Tanzania katika harakati za ukombozi wa bara la Afrika ikiwamo mchango wa Tanzania kumfanya Mandela na viongozi wengine wa Kiafrika kuonekana kama walivyoonekana kwenye macho ya dunia. 

Hakika, JK anastahili pongezi kwa kazi njema aliyoifanya leo ya kuiweka tena Tanzania katika ramani ya dunia, si tu kama nchi ile ya mbuga za wanyama na Mlima Kilimanjaro, bali ' Taifa Kubwa' lililochangia kushiriki mikakati ya ukombozi ikiwemo kutoa misaada ya silaha, mafunzo na hata makazi kwa wapigania ukombozi wa Afrika.

JK aliipitia historia ya mchango wa Tanzania ambayo wengi waliokuwa wakimsikiliza, ama waliisahau au hawakuijua kabisa.

Lakini, tujiulize pia kama Watanzania, katika aliyoyasema JK kule Quni, ni Watanzania wangapi wanayajua? Inahusu umuhimu wa kuipitia historia yetu ili, kama Watanzana, tuweze kumiliki ' K3'- Kujitambua, Kujiamini na kuthubutu. Imefika mahali tunaionea aibu hata historia yetu.

Na nyongeza katika yale aliyoyasema JK leo ni kumbukumbu ya kihistoria ambayo haitajwi pia, kuwa Baba wa Taifa , Mwalimu Nyerere, ndiye aliyempa hifadhi Tanzania, Rais wa Pili wa Afrika Kusini huru, Thabo Mbeki baada ya kutoroka Afrika Kusini. Baadae Thabo Mbeki akaenda kusoma Uingereza.

Jambo hilo linathibitishwa katika kitabu alichoandika msomi mahiri wa Afrika Kusini, William Gumede. Anasema;

" In 1962, Thabo slipped out of the country to which he would not return for twenty -eight years, travelling through Botswana to Rhodesia, where he was arrested and held in a Bulawayo prison for several weeks. The white Rhodesian authorities intended to deport him back to South Africa and waiting for security police, but British Labour MP, Barbara Castle intervened after being lobbied by the ANC, and Mbeki was granted asylum in Tanzania by President Julius Nyerere." ( William Gumede, Thabo Mbeki and The Search For Soul of The ANC, pg 36)

Naam, ni wakati sasa wa viongozi wengine, bila kujali itikadi zao, wanapokuwa kwenye majukwaa ya kimataifa, kuzitafuta fursa za kuonyesha yale ambayo huko nyuma tumekuwa na uwezo nayo, na bado, kama nchi, tunaweza kuaminika katika kutoa mchango wa uzoefu wetu kwenye masuala mbali mbali ya Kimataifa. 

Usiku Mwema.

Maggid Mjengwa.
Iringa.
Tags

Post a Comment

12 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Real it's AMAZING, tena kwa herufi kubwa, you ROCK JK

    ReplyDelete
  2. Prezdaa wangu anauza sana namuelewa sana jamaa!

    ReplyDelete
  3. Kweli kabisa rais wetu anajitaidi lkn wananchi hatuna shukrani siku Atakapomaliza muda wake ndipo tutakapojua thamani yakee.

    ReplyDelete
    Replies
    1. umeona ee ndipo watakapojuta kama waliby

      Delete
  4. Was nice speech for sure

    ReplyDelete
  5. luv you Jk.may God blec ya.

    ReplyDelete
  6. Kila mtu JK, JK! Ndiyo, speech ilikuwa nzuri lakini siyo yake (JK) ni alisoma kama vile mwl. wa Historia anavyosoma kitabu cha historia darasani. Hata familia ya Nyerer e ingeweza kusoma waraka huo. Acheni kuwa "pumba" , Viongozi TZ wanakuja na kuondoka infact baada ya miaka kumi ya uongozi bila kufanya lolote kwa wananchi na nchi ya Tanzania. Just give the credit for those who put the speech together than to the messenger! Wake up People.

    ReplyDelete
    Replies
    1. mdau kwa upande mwingine ntakubaliana nawe..hakuna watu wanafiki kama watanzania duniani. ukifanya jambo jema leo watakusifia kesho teleza tu kidogo, utasikia sijahi ona uongozi mbovu kama wa JK. Tatizo watanzania wengi hatupendi kufanya kazi, tuna ndoto za ghafla kesho kupambazuke tz iwe kama ulaya....meeen!mnajua walikopitia hadi kufika walikofka?niliona nyumba za miaka ya 1300 uholanzi ni nzuri sana, ila zimeachwa kama makumbusho. Tujiulize miaka hiyo sis tulikuwa wapi?kila leo utaona watu wakiifananisha tz na USA....haahahh itafika kipindi nasi tutafikia huko cha msingi ni kuongeza juhudi ktk kazi

      Delete
    2. ni kweli kabisa its just an history that was there anybody who knows how to memorize can say or read and speak aloud to the world to hear,,hivyo cha muhimu ni kuangalia yeye mwenyewe akija kuambiwa asome au aseme historia ya aliyoyafanyia TZ tangu awe kiongozi kweli atasema nini<< Zaidi atakuwa anajimumunya mumunya tu,,,,walking dead,,,i love him as a human but I totally hate him as a president..

      Delete
  7. samahani lakin. chuki hazijengi wabongo wanataka had chu** wanunuliwe na serikali. hao unaodhani watakusaidie wasubir xaaaaaana.kuna baadhi ya mifumo ipo tu hata kama tungekuchagua wewe ucngefanya kitu. fanya kazi kwa bidii ucsahau sala utatoka. wewe ni boss wa maisha yako japo serikar inahucka kwa nafac yake.

    ReplyDelete
  8. Tutaishi kwa hotuba nzuri jukwaani?. Eti hotuba ilifunika. Labda ilikufunika wewe

    ReplyDelete
    Replies
    1. hahahahaha nakubalina na wewe !! hotuba nzuri zisizo na mpango,,,
      cha asiingeenda kutoa hotuba halafu atupe mtirirko wa aliyoyafanya bongo yetu hii ,

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad