‘SAUZI’ YAMTAFUTA MKALIMANI FEKI WA VIZIWI KWENYE IBADA YA KUMKUMBUKA MANDELA

AFRIKA Kusini inamtafuta mkalimani feki wa kutumia ishara za viziwi ambaye alishindwa kufasiri walichokisema viongozi mbalimbali kutoka duniani wakati wa ibada ya kumkumbuka  aliyekuwa rais wa nchi hiyo Nelson Mandela iliyofanyika Jumanne wiki hii.

Mtu huyo asiyefahamika na aliyekuwa na pasi zilizotolewa kwa ajili ya usalama eneo hilo, alikuwa amesimama karibu na viongozi hao wakati wanahutubia katika uwanja wa Soccer City wenye uwezo wa kuingiza watu 95,000 ambapo jamaa huyo alionekana akifasiri lugha mbalimbali kimakosa.

“Ulikuwa ni upuuzi mtupu, hakupatia chochote na alishindwa hata kutoa alama ya kusema ‘asante’,” alisema  Delphin Hlungwane, mkalimani wa ishara wa chama cha viziwi cha Afrika Kusini ( DeafSA) ambacho kimelaani tukio hilo.

Pamoja na kwamba serikali ya nchi hiyo ilikuwa msimamizi wa sherehe hiyo, lakini jamaa huyo asiyefahamika mwaka jana alifanya hivyohivyo kwenye mkutano wa chama cha African National Congress cha nchini humo ambapo Rais Jacob Zuma alikuwa anahutubia.

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hakuwa feki lakini alikuwa anatafsiri kwa Kizulu sasa kama kiziwi alikuwa hajui kizulu ataelewaje anachosema Obama...? Au akama kiziwi mswahili na Obama anaongea Kiingereza angeelewaje..? hao watu wanaosikia Kiingereza hawakielewi sembuse viziwi...

    ReplyDelete
  2. Hahaha ndugu yangu nimefurahia comment yako hapo juu, ni kweli tupo wengi tunasikiya kingereza ila hatukielewi kabisa apo hujakosea. Ila nawapa pole sana viziwi kwakuletewa mkalimali feki

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad