SINEMA ZA KIBONGO LINI ZITABADILIKA?

KWENU,
Watayarishaji wa sinema za Kibongo. Hongereni sana na kazi. Mimi nipo sawa na mishe zangu zinaendelea vyema kabisa. Leo nimewakumbuka kwa barua kwa lengo la kuwekana sawa kidogo.
Ni kweli kuna tofauti kubwa sana katika sinema zetu za sasa na zile za miaka mitano iliyopita lakini kiukweli bado kuna changamoto nyingi.  Kuna makosa mengi madogomadogo ambayo yanaachwa na yanaweza kuondolewa na kufanya sinema kuwa nzuri ya kuvutia.

Huko nyuma makosa yalikuwa mengi sana; taa, picha, hadithi na mengine lakini sasa kidogo  yamepungua kwa kiasi kikubwa. 
Ndugu zangu, soko la sinema hivi sasa limepanuka. Ni ajira inayojitosheleza, tujitahidi kuondoa kasoro ndogondogo ambazo zinaweza kuondolewa na kuifanya sinema kuwa bora. Nimeona mengi lakini yenye umuhimu zaidi ni haya;

UHUSIKA/UHALISIA
Bado kuna makosa ya msanii kuvaa uhusika katika uhalisia wa tukio sawasawa. Makosa haya, zaidi yameonekana katika namna ambavyo stori inavyomhitaji msanii. Utakuta msanii anaigiza yupo kijijini lakini eti ameweka nywele wave au ametokelezea na pamba za kijanja.

Tabia ya kuwafanya walinzi wa getini kama machizi, bado inaendelea. Aliyewaambia kuwa kila mlinzi anayekaa getini ni komediani ni nani? Bado kuna tatizo hapa.

MWENDELEZO
Hata mastaa kabisa wanashindwa namna ya kudhibiti hili. Msanii amecheza amevaa nguo fulani, siku ileile kwenye tukio lingine anaonekana amevaa nguo nyingine, tena akiwa na mtindo mwingine wa nywele!
Lakini pia kumekuwa na tatizo la msanii kurudia nguo moja mara nyingi, hata kama stori inaeleza kuwa tukio linalofuata ni BAADA YA MIAKA MITATU! Hii siyo sahihi. Halafu inawezekana vipi msanii akaigiza akiwa amenyoa nywele staili moja mwanzo hadi mwisho?

Hilo linawezekana, lakini ni kwenye visa vinavyoonesha kweli kiliisha ndani ya siku moja. Mfano mzuri ni Sinema ya Swahiba. Ni kisa kizuri, kinaanzia mchana wa siku moja na kuishia asubuhi ya siku inayofuata. 
Mwanamke amesuka rasta katika mtindo fulani, basi ataonekana hivyohivyo, mwanzo hadi mwisho wa filamu. Hiyo siyo sahihi hata kidogo. Jitahidini muwe makini katika eneo la mwendelezo (continuity) ili kufanya sinema zenu kuwa zenye ubora.

MATUKIO YA KUCHOSHA!
Hili limelalamikiwa sana. Kwanza, sinema nyingi utakuta zina sehemu mbili (Part 1 & 11), lakini ukiingia sehemu ya pili, hakuna kitu. Ni marudio tu ya kilichoonekana sehemu ya kwanza au kurefusha matukio bila sababu.
Mfano, unaweza ukakuta kipande kinachukua mpaka robo saa. Mtu anaonekana anaamka. Anajinyoosha. Anajiangalia kwenye kioo. Anakwenda bafuni, unasikia maji yakimwagika. Anatoka. Anajikausha. Anavaa kisha anatoka nje na kuingia kwenye gari.

Hii haiko sawa. Kwani lengo la kufanya hayo yote ni nini? Lazima kila onesho (scene) liwe na sababu. Mfano, kama unataka kumuonesha mhusika akiamka, basi kuna sababu, kama kuangalia saa na kugundua amechelewa kazini, kumkosa mwenzake kitandani n.k.

Lazima kuwe na sababu. Wengine mnafurahisha kweli! Mhusika ataingia kwenye gari na bado ataonekana akiendesha barabara nzima mpaka anaingia ofisini... ni robo saa nzima! Yapo mengi lakini haya machache mkiyarekebisha mtapaisha filamu za Kibongo.

Uamuzi wa kupokea au kuacha, uko mikononi mwenu wenyewe! Kazi kwenu.

Yuleyule,
Mkweli daima,
GPL

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Apo umesema mwandishi, zinaboa sometime hizi bongo movies

    ReplyDelete
  2. me niliacha zamani kucheki hizo muvi

    ReplyDelete
  3. Mwanangu inabidi uwe Producer uwafundishe awa jamaa sababu ata mi nawaona wanaekti movie lakini awana ufahamu na fani hii na wengine unawaona kabisa katika izo movie zao wanaekti feki sana mpaka mtu unagundua na wengine limradi tuu waonekane..Mi nafikiri izi bongo movie ni njia tuu ya kupita na kujionyesha katika macho ya watu ili wajulikane na wafanye yale ya kweli yaliokuwa nalengo yao..Nyie bongo movie actor msipokuwa serious baada ya muda mtapoteza status yote na interest yote sababu sasa ivi kila mtu analalamika na movie zao...

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad