WAMEIBOMOA Gor Mahia. Ndivyo unavyoweza kusema kuhusiana na hatua ya Simba ya Tanzania kuwasajili kipa, Ivo Mapunda na beki Donaldi Musoti.
Klabu hiyo ya Tanzania ambayo maofisa wake walikuwapo jijini Nairobi wakati wa mashindano ya Cecafa Senior Challenge Cup yaliyomalizika juzi Alhamisi, walikamilisha usajili wa wawili hao jana Ijumaa.
Mapunda aling’ara katika michuano hiyo akiwa na timu ya Tanzania Bara, wakati Musoti alikuwa katika kikosi cha Kenya. Mapunda amesaini mkataba wa mwaka mmoja na nusu wakati Musoti amesaini miaka miwili.
Musoti alisema: “Nimefurahi sana kusaini Simba, nakwenda kufanya kazi na Loga (Zdravko Logarusic) ambaye nimekaa naye Gor Mahia kwa mafanikio.
“Nina uzoefu wa kutosha na soka la Afrika Mashariki na ninadhani nitafanya kazi nzuri na Simba kama Wakenya wenzangu waliopita, kikubwa ni ushirikiano tu.”
Katika kikosi cha Gor Mahia,Musoti hucheza sambamba na Ivan Anguyo au Edwin Lavatsa.
Makamu Mwenyekiti wa Kwanza wa Gor Mahia, Faz Ochieng, amekiri kuwa kuondoka kwa wawili hao ni pigo kwao na watakaa kujadiliana nini cha kufanya.
“Sijapata taarifa rasmi za kuondoka kwao, lakini mikataba yao inamalizika mwezi huu na ilikuwa tukae nao kujadiliana juu ya mikataba mipya,” alisema.
Gor Mahia itakuwa imepata pigo kubwa baada ya wachezaji hao kusaini Simba kwani walikuwa tegemeo kwao na waliibeba kwenye Ligi Kuu Kenya msimu uliomalizika ambapo timu hiyo ilitwaa ubingwa.
Mapema wiki hii matajiri wa Gor Mahia walijinadi kuwa watahakikisha kwa gharama yoyote ile wanawabakiza wachezaji hao jambo ambalo limegonga mwamba kwani viongozi wa Simba waliowasili usiku wa Jumanne iliyopita wameshamaliza kazi.
Kuthibitisha jinsi klabu hiyo ilivyopata pigo, baadhi ya mashabiki wa Gor Mahia jana Ijumaa walivamia ofisi za timu hiyo zilizopo maeneo ya uwanja wa soka wa Nyayo wakiwa na mavuvuzela na kuwapigia kelele viongozi wao wakiwahoji imekuwaje wamewaachia wawili hao kujiunga na Simba.
Mashabiki hao waliokuwa zaidi ya 50 wamechukizwa na jambo hilo na kuwaoana viongozi wao ni wazembe kwani klabu hiyo ni kubwana ina fedha za kuwabakiza.
Afadhali ya huyo Mkenya, ila Ivo amekosea sana kuja simba, sijui diference ya mkwanja, ila Simba hakuna soka, kuna majungu
ReplyDeleteKama amekuja kupiga majungu, haya ila simba na yanga sio timu