Stori: Gladness Mallya na Hamida Hassan
SIKU chache baada ya ndoa ya mastaa wawili wa filamu Bongo, Salome Ndumbagwe Misayo ‘Thea’ na Michael Sangu ‘Mike’ kuvunjika, imedaiwa mambo ya kishirikina yanahusika kwani mauzauza yalianza siku nyingi zilizopita.
Mtu wa karibu wa mastaa hao aliyeomba jina lake liwekwe kapuni alidai kuwa mara kadhaa wasanii hao wamekuwa wakikumbwa na mambo ya ajabu yaliyoashiria kuwa ndoa yao haina uhai.
“Unajua kwa nyakati tofauti pete za ndoa za Thea na Mike ziliwahi kuwatoka kiajabu vidoleni wakiwa chooni. Haikuwa jambo la kawaida na wenyewe walishituka na kukosa amani,” alisema mtoa habari huyo.
Hata hivyo, wahusika wamekuwa wakiamini kuvunjika kwa ndoa yao ni mipango ya Mungu licha ya Mike kuhisi kuwepo kwa nguvu za giza katika kuachana kwao.
“Mimi naamini kila linalotokea ni mipango ya Mungu lakini katika hili mmh, napata mashaka,” alisema Mike.
Naye The alisema: Mungu hakupanga tu tuendelee kuwa kwenye ndoa, kwa hiyo limetokea na maisha yanaendelea.”
Chanzo:Global P
hawa bongo movie wangeendelea kuwekana vimada tu coz kudumu kwenye ndoa walishashindwa....poleni na imani zenu zakishirikina.
ReplyDeleteKuwa na akil wewe Thea Mpango wa Mungu kwenye ndoa n kwamba wa2 waishi mpaka kifo. Sio kuacha nisha. huo ni umalaya wenu na upuuzi wenu bongo move hamdumu kwenye ndoa. Ukimtoa sajuki na wastara
Deleteacha ujinga
ReplyDeleteNawashauri hao wanandoa si ni master, wamuone mtaalam Shamim Mwasha (Mrs. Abdul Nsembo) wa mambo ya kishirikina akawaonyeshe anakonyoosha mambo yake. Huyu dada ni kigaga sana hapa mjini, anaweza kuwasaidia na mambo yao yakaenda muruwa.
ReplyDeleteToa pumba hapa shetani mkubwa wewe
DeleteAcha ujinga w kama unamaugomvi yako personal na shamimu usiyalete hapa we ulijuaje kiganga kama haumsindikizi kwanza nyie ndo wenye wivu ulitaka huyo abdul akuoe ww nn mxuuuuuu ujinga na wivu tu ndo umekutawala
DeleteNafikiri tumwachie MUNGU ila zingine ni laana za mahusiano ya awali,Thea aliwahi kuishi na jamaa mmoja kule Tabata Mawenzi na kuzaa naye mtoto aitwaye Maron na baadae thea akamtosa jamaa vibaya baada ya kupata jina katika sanaa!
ReplyDeleteHiyo move yao inaitwaje naona ni mpya
ReplyDeleteinaitwa ndoa ndoano, ndio imetoka kama cku mbili hiv zilizopita
Deleteinaitwa ndoa ndoano, ndio imetoka kama cku mbili hiv zilizopita
DeleteMh pole yao
ReplyDeletepoleni wapendwa bt c mpango wa mungu ni wenu na ndugu yenu shetani,mungu hawezi kuwatenganisha ktk ndoa
ReplyDelete