TRENI YA MWAKYEMBE YAOKOA SHILINGI BILION 3

Wakati taarifa mbalimbali zikieleza kuwa treni ya usafiri jijini Dar es Salaam, maarufu kama ‘Treni ya Mwakyembe’ inaingia hasara ya milioni 2.1 kwa siku kutokana na gharama za uendeshaji, Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe amekanusha taarifa hizo na kusema, treni hiyo imepunguza hasara ya zaidi ya Sh3 bilioni.

Mwakyembe alisema uwepo wa usafiri huo umesaidia kupunguza msongamano mkubwa jijini, ambao unasababisha hasara ya Sh3 bilioni ambazo ni matokeo ya kukaa barabarani kwa muda mrefu, kuchelewa kazini na katika majukumu mengine pamoja na upotevu wa nishati.

Akizungumza katika Kongamano la miundombinu na uchukuzi katika Nchi za Mabonde ya Ufa uliofanyika jana jijini, Mwakyembe alisema hatasita kuendelea kuwekeza fedha zaidi katika reli, kwani ana uhakika ina faida kubwa na imesaidia katika uchumi na kijamii.

“Ukitaka kujua reli ni ya muhimu, tangaza leo kuwa unasitisha usafiri huo, utaona jinsi ambavyo watu watahangika na shida ya usafiri,” alisema.

Mwakyembe alisema, ukilinganisha hasara inayopatikana katika gharama za uendeshaji zinazotajwa na kiwango cha hasara kinachopunguzwa katika mtazamo wa uchumi na shughuli za maendeleo jijini, ni bora reli hiyo iwepo daima.

Waziri Mwakyembe alisema ana mipango mikubwa ya kuuboresha usafiri huo ingawa ni mapema mno kuiweka wazi kwa sasa.

Alisema mabasi zaidi ya 500 yameondoka barabarani, hivyo kupunguza msongamano.

Alisema treni hiyo itaimarishwa ambapo mabehewa mapya ya kisasa yanatarajiwa kuletwa.

Hata hivyo kutokana na ufinyu wa bajeti, Wizara ya Uchukuzi inatazamia kupata mwekezaji, ambaye anaweza kuwekeza katika treni hiyo na kusaidia kupatikana kwa treni ya kisasa zaidi inayofaa kwa matumizi ya mjini.

Kwa sasa mabahewa yaliyopo ni ya kizamani, ingawa yanasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza adha za usafiri.

Julai mwaka huu, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Reli Tanzania, Kipalo Kisamfu alisema treni hiyo inaingiza hasara ya 1.2 milioni kwa siku kutokana na gharama kubwa za uendeshaji, ikiwemo vitendea kazi ambavyo siyo maalum kwa treni za mijini.
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. HUYO MKURUGEZI KANUNULIWA ILI AMPIGE VITA MWAKYEMBE ASHINDWE NA ALEGEE MAANA TRENI NDIO MKOMBOZI WETU KUMANINA ZAKE

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad