WABUNGE WAZIDI KUMWANDAMA WAZIRI MKUU PINDA

Mzimu wa kung’olewa unazidi kumwandama Waziri Mkuu, Mizengo Pinda huku Mbunge wa Muhambwe, Felix Mkosamali (NCCR), akitaka Bunge lipige kura ya kutokuwa na imani naye.

Akizungumza bungeni mjini Dodoma jana, mbunge huyo alienda mbali zaidi na kuomba Naibu Spika, Job Ndugai kuwaongoza wabunge kupiga kura hiyo ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu.

Pia alitaka kung’olewa kwa Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Hawa Ghasia akisema haiwezekani aendelee kuwepo wakati fedha za wafadhili zinaliwa bila yeye kuchukua hatua.

Mkosamali anakuwa mbunge wa tatu kupendekeza kung’olewa kwa waziri mkuu, akitanguliwa na Mbunge wa Mwibara, alphaxard Lugola (CCM) na Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR).

Mkosamali alisema ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) zinaonyesha hakuna ufuatiliaji wa fedha zinazoidhinishwa na Bunge na kupelekwa katika Halmashauri nchini.

Alisema taarifa zinaonyesha asilimia 20 ya bajeti ya Serikali huingia mifukoni mwa watu na kuongeza kuwa hata Bunge likapitisha bajeti ya Trilioni 40 bado asilimia 20 zitakwenda mifukoni mwa watu.

Mkosamali alisema katika semina mbalimbali wabunge walielezwa kuwa taarifa za CAG zinazofichua ufisadi wa kutisha pamoja na taarifa za Kamati za Bunge zimekuwa hazifanyiwi kazi na Serikali.

Mbunge huyo aliwasihi wabunge wenzake kuchukua hatua na kuhakikisha kuwa kabla ya kumalizika kwa mkutano wa 14 wa Bunge unaoendelea mjini Dodoma mawaziri kadhaa wawe wameng’oka.

Akinukuu Ibara ya 52 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977, Mkosamali alisema, Waziri Mkuu ndiye atakuwa na madaraka ya juu katika udhibiti na usimamizi wa Serikali.

Aliongeza kusema “Kwa nini tusipige kura ya kumwondoa?... Mheshimiwa Naibu Spika wewe kama kiongozi wetu ndio unapaswa kutuongoza kupiga kura ya kuwaondoa hawa watu.”

Mkosamali alisema wabunge wanatoa mapendekezo hayo kwa vile wameshindwa kufanya kazi ambayo walipatiwa na kusisitiza kuwa wameshawapima na kubaini kuwa hawawezi kazi tena.

“Hatuna chuki na mtu….Hata tukiwaambia tunajua hamtafanya tumeshawapima tunajua hamtaweza sasa tunawashauri nini tena?” alihoji Mkosamali wakati akijenga msingi wa hoja yake hiyo.

Mbunge wa Viti Maalum, Pauline Gekul (Chadema), alisema ni vizuri mkuu akaondoka mapema na mawaziri wake walioshindwa kazi na ambao wamepuuza ushauri na mapendekezo ya Bunge.

Hata hivyo Gekul alisema kuwang’oa Pinda, Ghasia na mawaziri mizigo hakutasaidia kwani mfumo mzima wa serikali umegubikwa na rushwa na kwamba suluhisho pekee ni kuing’oa CCM madarakani.

“Wataanzania waadhibu CCM kwa kuwaondoa kwenye masunduku ya kura kwa sababu hata wakiletwa wengine(mawaziri)bado mfumo wa rushwa ni ule ule na CCM kimeshindwa kuikemea Serikali” alisema.

Akizungumzia suala la mishahara hewa, alisema waziri Ghasia aliwahi kuliambia Bunge kwamba ameanzisha mfumo wa Epica na kwamba suala la kuwapo malipo hewa ya mishahara litakuwa ndoto.

“Lakini katika ripoti hii 1.5 bilioni zimelipwa kama mishahara hewa imeliwa katika ngazi ya Halmashauri, kwani Mheshimiwa Waziri (Ghasia) usiwajibike? alihoji Mbunge huyo.

Alisema mbali na malipo hayo, lakini yapo malipo mengine ya Sh693 milioni…. Hizi fedha zingeweza kuwalipa walimu 1,400 posho za mazingira magumu ya sh500,000 kila mmoja”alisema Gikul.

Katika mchango wake huo alionekana kuishambulia zaidi Serikali ya CCM kwamba imeshindwa kuongoza nchi, hali ambayo ilimuinua kwenye kiti chake Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai.

“Tunafika mahali ambapo hatuelewani naomba tujielekeze kujadili taarifa za kamati tatu badala ya kujadili ripoti ya CAG japo siwafungi kujadili jambo lililo nje ya hili”alisema Ndugai.

Gekul alisema kinachojadiliwa ni pamoja na taarifa ya kamati ya Serikali za Mitaa (Laac) na imekuwa ikieleza yale yale aliyokuwa akisema na taarifa ya kamati hiyo nayo imeegemea ripoti ya CAG.

Hata hivyo baada ya kumaliza kuchangia, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu(Sera,Uratibu na Bunge), William Lukuvi alisimama na kudai mchango wa Gekul ulivunja kanuni ya 64(1) ya Bunge.

“Nimemvumilia sana Mbunge wa viti maalum sikutaka kumkatisha dada yangu katika hotuba yake… Sio kwamba sisi hatuwezi kusema lakini katika hotuba yake yote amevunja kanuni ya 64”alisema.

Alisema kanuni hiyo inasema Mbunge hatazungumzia jambo ambalo haliko kwenye mjadala kwa sababu yote anayozungumza hapa hayapo kwenye hotuba…amezungumza matusi makubwa”alisema.
-Mwananchi


Tags

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ccm oyeee! mtuache kabisa na chama chetu kilichotunzia amani kwa zaidi ya miaka 50, hivyo vyama vyenu vya udini na ukanda peleka huko si tumeridhika na umaskini wetu, wacha ninywe chai na chapati niwahi dala dala.

    ReplyDelete
    Replies
    1. heheheh umeona ee

      Delete
    2. Kunywa chai na chapati then ukafirwe kumamamamamamamako!!!!!

      Delete
  2. hakuna hatuwa mbaya katika misha ya mwanadamu kama hatuwa ya KUJISAHAU yeye mwenye pamoja na mambo yote hayo bado unadiriki kupamba mahovu kwanini watu munaishi kinafki namna hii

    ReplyDelete
  3. KUMAMAYE UMEZOEA UMACKN?

    ReplyDelete
  4. Huyo ni kuma, anatombwa ili apate hela ya kunywa hiyo chai na chapati, hana lolote huyo mwanaharamu CCM, kafie mbali.

    ReplyDelete
  5. Wewe Lukuvi ni lazima utetee mafisadi ili ujinusuru na mkono wa sheria usibanwe na kuhojiwa ulikopata mabilioni ya kununua lile jumba lako la kifahari pale mbezi beach mtaa wa colonel mitha.Umesita kuhamia ,unaogopa nini,jaribu kuhamia uone utakavyo chanwa live fisadi wewe.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad