WAFANYAKAZI WAWILI WA UWANJA WA KIA MBARONI KWA MADAWA YA KULEVYA

Wafanyakazi wawili wa kampuni ya uwakala wa uendeshaji wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa kilimanjaro (KADCO), wanashikiliwa Polisi kwa madai ya kupanga njama za kupitisha wasafirishaji wa dawa za kulevya katika uwanja huo.
Taarifa kutoka katika uwanja huo, zilidai kuwa wafanyakazi hao, ndio waliohusika kusafirisha watuhumiwa hao raia wa Nigeria na Liberia mpaka katika uwanja huo na walifika saa 9 mchana Jumamosi iliyopita.
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari kutoka uwanjani hapo, wanawake hao wawili walitumia gari aina ya Noah, linalodaiwa kumilikiwa na mmoja wa wafanyakazi hao.
Mtoa habari wetu alidai kuwa baada ya kufikisha wageni hao uwanjani, mwanamke Mnigeria aliyekuwa na kilo 10 za dawa hizo, aliandaliwa mazingira ya kupita uwanjani hapo bila kukaguliwa, lakini kwa bahati mbaya alikuwa ameshachelewa ndege.
Kutokana na hali hiyo, aliandaliwa usafiri mwingine wa Shirika la Ndege la Precision kwenda Nairobi kuanzia saa 11 alfajiri ya juzi. Mwenzake Mliberia anayedaiwa kuwa na kilo tano za dawa hizo, aliandaliwa usafiri wa Shirika la Ndege la Ethiopia na alitarajiwa kuondoka uwanjani hapo saa tisa usiku wa kuamkia juzi pia.
Taarifa hizo zilidai kuwa wafanyakazi hao kwa kuwa hawakuwa zamu usiku, walikabidhi wageni hao kwa mfanyakazi mwenzao na kumlipa ili asaidie wapite uwanjani hapo bila kukamatwa
Source: Habari Leo

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. mbona hujaeleza kama wanawake hao wawili walikamatwa!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad