"WAJINGA USEMA KWAMBA CCM NDIO ILILETA UHURU TANGANYIKA" PROF MBELE

Kiwango cha ujinga Tanzania kinatisha. Utawasikia wengi wakisema kuwa CCM ilileta Uhuru Tanganyika mwaka 1961.

Wajinga wengine, kuanzia wanasiasa hadi watu wa mitaani, husema kuwa CCM imekuwa madarakani kwa miaka 52.Utamsikia mwanasiasa anaiponda CCM kwa kuuliza, "Miaka yote 52 ya utawala wa CCM, wananchi mmenufaika vipi?" 

Na utammsikia kada wa CCM akitamba, "CCM ni chama chenye uzoefu wa miaka 52.

Hapakuwa na CCM mwaka 1961. Chama kilicholeta Uhuru Tanganyika ni TANU. Wala CCM haijawa madarakani miaka 52. Kuna mengi katika historia ya Tanganyika na Tanzania ambayo yanasahaulika au kupotoshwa kwa sababu ya uzembe wa wa-Tanzania.

Wajinga wengine wanasema kuwa tunasherehekea kumbukumbu ya Uhuru wa Tanzania au Tanzania Bara. Mwaka 1961 hapakuwa na nchi iliyoitwa Tanzania wala Tanzania Bara. Nchi iliyopata Uhuru mwaka ule ni Tanganyika. Inasikitisha.
Tags

Post a Comment

15 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. ulikuwa wapi siku zote kutoa elimu hiyo?mjinga anaitaji kuelimishwa sio kumponda utakuwa hujasaidia kitu na u profesa wako.

    ReplyDelete
  2. WE MZEE MNAFKI MIAKA YOTE HUJAELIMISHA UMEWASHWA NA NN LEO OVYO AFU UNAPOND MPSIIIIIIIIIII!!!!!!!! CJUI ULIKUW WAPI ENZ IZO MBURULA WEWE.

    ReplyDelete
  3. Dah kweli uyasemayo lakin ulikuwa wapi?

    ReplyDelete
  4. te te! teh! mi napita tu!

    ReplyDelete
  5. te te! teh! yaani profesa ni mburula daaah mi napita tu!

    ReplyDelete
  6. Makubwa haya ww ucyekuwa mburula ulikua wap cku zote kutujuza?

    ReplyDelete
  7. kwa hiyo unatushaurije

    ReplyDelete
  8. Profesa amekula pilipili zinamuwasha mpaka matakoni na anahitaji kukunwa huyu.............?

    ReplyDelete
  9. wajinga ni ccm, sababu ndo wanatamba hivyo.

    ReplyDelete
  10. Kosa la prof likowap! najua amewaotea wajinga..

    ReplyDelete
  11. afadhali umetujuza

    ReplyDelete
  12. Hukuchelewa professor,wa- Tanzania tunahitaji kuelewesha wengi upeo mdogo na ndio wajinga wa kwanza kukoment ujinga Wao,wanaohitaji kuelewa wataelewa,jitokezen wengi semeni msiogope,najua küna mengi Tanzania/tanganyika hayajaongelewa....big jp professor Mzee Kwa usubutu Wako,chant dem babilon.möre fire!!

    ReplyDelete
  13. we profesa we si mtanzania ? kamamtanzania we ni profesa wa wajinga kwahiyo wewe kubwa lao yaani una profa jinga. we siumesoma zama za nyerere elimu bure mpaka ukawa prof sasa nini tena au ndio unataka kutoka si kiivyo we boga tu . ushachoka utatuletea mambo ya miaka ile . we badala ushukuru ulisoma bureeeee saiv unaponda watanzania wajinga mjinga mwenyewe prof boga

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad