"WALIOHUSIKA KUCHOMA MOTO OFISI ZA CHADEMA NI CHADEMA WENYEWE..." TAMKO LA POLISI BAADA YA UCHUNGUZI KUKAMILIKA

Polisi mkoani Arusha imekamilisha uchunguzi wake kuhusiana na kuungua kwa Ofisi za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kusema wanachama wa chama hicho ndio waliohusika. 

Hata hivyo, Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema amepinga kauli hiyo na kulipa jeshi hilo siku nne kuwakamata na kuwahoji watuhumiwa watano baada ya kulipatia majina hayo akidai kuwa ndio wanaohusika na uchomaji moto ofisi za chama hicho.

“Tumewapatia polisi majina... tunaamini walihusika moja kwa moja la sivyo, chama kitatumia vijana wetu wa Red Brigade kuwakamata na kuwafikisha polisi,” Lema aliwaambia waandishi wa habari jana.

Ofisi za Chadema zilizoko katika eneo la Ngarenaro, zilinusurika kuteketea kwa moto juzi baada ya watu wasiojulikana kuwasha moto katika moja ya vyumba vyake.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Arusha, Japhet Lusinga alisema:

“Katika uchunguzi wetu, tumebaini kuwa hakuna mahali palipovunjwa kutoka nje ya uzio na kuruhusu watu kuingia ndani... tumegundua kuna tundu dogo darini eneo la kuelekea bafuni la upana wa futi moja na nusu kiasi haliwezi kuruhusu mtu kupita.

“Tumejiridhisha kuwa hakuna mtu anayeweza kupita hapo na ndani tulikuta majivu na baadhi ya vitu vilivyoungua na vifaa vingine.”

Lema akiwa na Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Arusha, Ephata Nanyaro alisema: “Tumebaini polisi wanataka kulifanya jambo hili kama la siasa ndiyo sababu juzi badala ya kuanza kuchunguza waliohusika, waliwakamata Mtunza Ofisi na mlinzi wetu na kuwalaza rumande hadi leo (jana) asubuhi kwa madai eti wanawahoji.

“Hatukubaliani na taarifa yao, hii ni siasa. Kulitokea mauaji ya bomu, wakasema Chadema wamejilipua, leo ofisi imechomwa wanasema Chadema wenyewe, hili hatukubali, “ alisema.

Msajili alaani
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi amelaani tukio la kuchomwa moto ofisi hizo za Chadema na kusisitiza kuwa wananchi hususan wanasiasa wasiwe wepesi kuingiza hisia kwenye makosa ya kijinai.

Alisema kuwa tukio hilo linapaswa kukemewa kwa hali yoyote ile kwa kuwa linavuruga na kuhatarisha amani ya nchi.
Tags

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. mchawi wako ni wewe mwenyewe hahaha

    ReplyDelete
    Replies
    1. Halafu eti wanataka kuongoza nchi

      Delete
  2. Lema akamatwe kwanza yy,maana anajifanya anajua kila kitu mjinga wa akili bange tu zinazomuendesha,na mwisho wa chadema umefika,eti wanataka kuongoza nchi

    ReplyDelete
    Replies
    1. wataiweza mambulula hawa nchi mchezo aendelee kuongoza bunge la wachaga tu ndo wanaweza

      Delete
  3. Hatu like tena peg yako ya kisenge! Admin huna akir,kila mada unayoleta,hutaki michango ya wadau,unacomment upumbavu mtupu!

    ReplyDelete
  4. ACHENI UNAFIKI UKIFIKIRIA WANACHOMA ILI IWEJE?HUO NI UCCM MPAKA POLISI

    ReplyDelete
  5. Katika jambo hili polisi wametoa majibu haraka sana, ikifikiria vizuri ni kama majibu walikuwa nayo. Kama mwanafunzi anae ingia kufanya mtihani ambao maswali alikiwa nayo kwa wiki nzima iliyopita. Hapo tutegemee kitu gani? Tafakari....

    ReplyDelete
  6. we lema na wenzako iyo sio siasa bali ni kushindwa siasa mnatuaribia mali zetu kwa kuzichoma moto alafu mnasingizia ccm sio kweli punguzeni kuvuta bangi me ni chadema lakini napingana na nyie mbon huku dar hakuna ujinga huo msijitafutie umaarufu kiivyo kachome nyumba ya familia yako moshi kama kweli unataka umaarufu

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad