ZIARA YA KATIBU MKUU DK WILLIBROD SLAA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Willibrod Slaa ataanza ziara ya siku 20 katika mikoa ya Shinyanga, Kigoma, Tabora na Singida kuanzia Desemba 4-23, mwaka huu.

Lengo la ziara hiyo ambayo imetokana na maombi ya muda mrefu ya viongozi wa chama katika maeneo husika, ni kuimarisha na kukagua uhai wa chama katika ngazi za chini hususan kata na majimbo mikoa hiyo.

Katika ziara hiyo, Katibu Mkuu Dkt. Slaa atakutana na wananchi katika mikutano ya hadhara ambapo atazungumzia masuala mbalimbali ya kitaifa na eneo husika, kisha atafanya vikao vya ndani vya kichama.

Ziara hiyo itaanzia mkoani Shinyanga ambapo siku ya Jumatano Desemba 4, mwaka huu, Katibu Mkuu Dkt. Slaa atakuwa Wilaya ya Kahama, siku inayofuata Desemba 5, atakuwa Wilaya ya Kakonko, Jimbo la Buyungu na Desemba 6, atakuwa Jimbo la Muhambwe.

Ratiba ya siku zinazofuata itaendelea kutolewa kwa vyombo vya habari.

Imetolewa Jumanne, Desemba 3, 2013, Dar es Salaam na;

Tumaini Makene
Ofisa Mwandamizi wa Habari CHADEMA
Tags

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hata Hai utumtaki!!!

    ReplyDelete
  2. Hawana jipya wadini na wakabila tu.

    ReplyDelete
  3. Uncle samy singida, ZITTO ni msaliti wa chama na achie ngazi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Fala Wewe Unajua Usaliti Wewe

      Delete
  4. Zito yuda msaliti.hatumtaki chadema.na nyie weu hapa atubembelez mtu kama vp na nyie mfuaten hicho kizito chenu ccm hapa hatutaki wafiki pumbv sn

    ReplyDelete
  5. Uncle samy singida. Kama unabisha nitokee kwa 0712420210 nikupe data zote za ZITTO ninazo na uhakika wote analivyopanga kukisaliti chama cha chadema, majimbo nengi yangepita 2010 lakn zitto alihucka kuangushwa kw chadema, na wa2 wa kigoma hawaelewi wanamwona zitto ni mwema kw maclahi yao 2 c kw wa tz wote nawashangaa kutomckiza katibu mkuu Dr SLAA

    ReplyDelete
  6. Tatizo Lenu Chadema Hamuujui Upinzan Ni Nini Mnakurupuka Tu. Na Chadema Ndo Ishakufa

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad