ZITTO: URAIS, MABILIONI YA USWISI VINANIMALIZA

Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe amesema tuhuma alizosomewa na uongozi wa Chadema katika kikao cha Kamati Kuu sizo zilizoelezwa na chama hicho mbele ya waandishi wa habari na viongozi wa chama hicho.
Aidha, amesema kuwa vita aliyopo siyo kati ya Chadema na Zitto, bali ni vita ya watu wengi, akitaja magenge ya watu wanaotaka urais 2015 na walioficha fedha nje ya nchi walioungana wakiona tatizo lao ni yeye hivyo kutaka kumwondoa bungeni.
Akizungumza katika mahojiano maalumu na gazeti hili kwa njia ya simu, Zitto alisema kuwa hadi sasa bado hajapokea tuhuma 11 anazokabiliwa nazo, hivyo hajui makosa hayo na bado anasubiri akabidhiwe kwa maandishi.
Ana ugomvi gani na viongozi wenzake?
Alipotakiwa kueleza iwapo ana ugomvi na watu ndani ya Chadema, Zitto alisema kuwa huenda mambo hayo yanatokea kwa sababu mahasimu wake wa kisiasa wa ndani na nje wameamua kuungana na kupambana naye ili kumdhoofisha kisiasa kwa masilahi yao.
Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. zitto unakichofanya it is of good cause, but remember human beings are difficult people hauwezi kumchunga binadamu ndio maana hata mungu katuumba na free will, kuna mabaya na mazuri sisi kama binadamu tunatakiwa kuchagua. Hao mafisadi you are so trying to bring them to light hata mungu anawaona lakini anasubiria siku ya hukumu watakipata cha mtema kuni. my dear zitto these guys are not good! please watch out! wanaweza hata............

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ninakuunga mkonoblogger wa Dsc 1st 1:53 am Kwa kuongezea ni kuendelea kumuunga mkono Mh. Zitto, kwasababu tuache kuongea tuu hii ni era ya vitendo -Umasikini umezidi TZ na ufisadi unaongezeka hasa kwa viongozi na ndugu na jamaa wa hao viongozi. Tuko pamoja Mh. Zitto.

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad