MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Zuberi Kabwe (MB) amewasilisha barua ya kupinga uamuzi wa Kamati Kuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wa kumvua nafasi zake za uongozi ndani ya chama hicho.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana jijini Dar es Salaam na Mwanasheria wa Zitto, Albert Msando akizungumza na waandishi wa habari, amesema tayari mteja wake ametoa taarifa kwa Katibu Mkuu wa Chadema kumjulisha nia yake ya kukata rufaa Baraza Kuu la Chama hicho kupinga hatua iliyochukuliwa na Kamati Kuu dhidi yake kumvua nyadhifa zake ndani ya Chama.
Msando amesema mteja wake amewasilisha sababu mbili za msingi za kukata rufaa; moja ikiwa ni Utaratibu wa kuchukua hatua za nidhamu ulikiukwa na ya pili ikiwa ni sababu za kuchukuliwa hatua hazi kuwa na mashiko.
“…Utaratibu ambao unatakiwa kufuatwa kabla ya kumchukulia hatua za kinidhamu kiongozi kwa mujibu wa Katiba na Kanuni za Uendeshaji ni kama ifuatavyo; Kanuni ya Uendeshaji 6.5.6 inasema; Kiongozi yeyote hatachukuliwa hatua za kinidhamu bila kwanza kupewa mashitaka yake kwa maandishi na mamlaka husika na kupewa nafasi ya kujibu mashitaka kwa maandishi.
“…Pia tunapenda ijulikane kwamba Kanuni ya Uendeshaji 6.5.2 (a), (b), (c) na (d) kama ilivyorekebiswa Januari 2013 inasema; Kwa mujibu wa ibara ya 5.4.3 na 5.4.4 ya Katiba mwanachama yeyote hatachukuliwa hatua za kinidhamu ama kuonywa ama kuachishwa ama kufukuzwa uanachama bila kwanza; a) Kujulishwa makosa yake kwa maandishi na kutakiwa kutoa
majibu katika muda usiopungua wiki mbili.”
“…b) Kupewa nafasi ya kujitetea mbele ya kikao kinachohusika. c) Mwanachama atajulishwa kwa maandishi uamuzi wa kikao mnamo wiki mbili baada ya kusikilizwa. d) Kamati Kuu inaweza kuchukua hatua za dharura bila kuzingatia utaratibu (b), (c) hapo juu kama itaona maslahi ya Chama kwa ujumla yanaweza kuathiriwa isipokuwa mwanachama au kiongozi anayelalamikiwa atalazimika kuitwa kwenye kikao husika,” alisema Msando akizungumza na waandishi wa habari.
Akizungumzia matukio ya vurugu na vitisho ambavyo baadhi ya viongozi wa Chadema wamekuwa wakipata kutoka kwa baadhi ya wanachama mikoani, hasa wanaofanya ziara za chama hicho, Msando amesema mteja wake hausiki na matukio hayo aliyoyaita ya kusikitisha ambayo mengine yamefikia mahali kuwa fujo na vurugu ikiwa ni pamoja na kurushiwa mawe Katibu Mkuu wa Chama.
“…Vurugu hizo baadhi zimehusishwa na Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe na baadhi ya watu. Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe hahusiki kwa njia yoyote na hayo yanayoendelea na anayakemea na kuwashauri wanachama wote kuwa watulivu na kuendelea kuwaheshimu viongozi wa kitaifa,” alisema mwanasheria Msando.
Huyu nae tulimuamini kumbe kuma tu ...Kibaraka wa nyinyi em...mkundu wake fala huyu
ReplyDeleteMwanaume anarudi huyo sasa watatoka akina Mboya,Slaa wezi tu wa pesa za ruzuku, Chadema ni Instute ya taifa mnataka kuifanya ya kikabila au sacos kama ndiyo hivyo kuweni wazi tu kama chama cha kaskazin tujue moja sisi wa songea
ReplyDelete