Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe amevunja ukimya na kusema hayuko tayari kwa sasa kuwataja Watanzania wenye mabilioni huko Uswisi na kuitaka Serikali ifanye uchunguzi.
Zitto ndiye aliyeibua hoja bungeni kuwa kuna Watanzania walioficha Sh315 bilioni katika taasisi za fedha nchini Uswisi.
Katika taarifa yake aliyoitoa jana, Zitto alisema anasita kutaja majina hayo sasa ili kuepusha kile alichosema majina hayo kutumiwa vibaya bila kujali kama Watanzania walizipata fedha hizo kihalali au la na kuzihifadhi nje ya nchi.
Alisema ameshauri mchunguzi wa kimataifa anafaa kufanya kazi hiyo.
Mbunge huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), amesema wastani wa Sh729.3 bilioni hutoroshwa kila mwaka kwenda nje ya nchi.
Alisema kauli ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Fredrick Werema kwamba yeye (Zitto) hakutoa ushirikiano wa kamati inayochunguza sakata hilo si ya kweli.
“Nataka niwahakikishie, nimekutana mara nne na kamati hii. Nimewapa mpaka jina la mchunguzi wa kimataifa atakayeweza kuwasaidia katika uchunguzi huu, leo naambiwa sitoi ushirikiano,” alisema Zitto.
Alisema mchunguzi huyo wa kimataifa ana uzoefu katika uchunguzi wa suala kama hilo na angeweza kuwatambua kwa majina na kiasi cha fedha na pia uhalali na uharamu wa fedha hizo.
Alisema ameshangazwa na hatua ya Serikali kumbeza pale alipopendekeza suala la kutafutwa mchunguzi wa kimataifa lakini siku chache baadaye ikatangaza magazetini nafasi ya kazi hiyo.
Tangazo hilo lilichapwa Desemba 17, mwaka huu siku ambayo Zitto alisema kwamba angesoma maelezo binafsi kujibu kauli ya Jaji Werema. Hata hivyo, alisema alikosa nafasi. Zitto amesema hashurutishwi na azimio la Bunge kutaja majina hayo kwa sababu yeye siyo chombo cha uchunguzi ambacho kinapaswa kuwa na mkono mrefu.
Alisema wakati akikabidhi majina ya Watanzania hao, angependa ushahidi huo uwe umefanyiwa uhakiki na vyanzo vyake vya kimataifa na vyombo vya usalama vya Serikali nchini.
“Siko tayari kutaja kwa sasa. Narudia tena kwa sasa hayo majina maana naweza kusababisha wahukumiwe na umma bila kupitia utaratibu uliowekwa na sheria zetu hapa nchini,” alisema Zitto.
ZITTO:SIWATAJI WALIOFICHA MABILION USWISI NG'O
6
December 28, 2013
Tags
haa yamekuwa hayo@ duu
ReplyDeleteBwege mtozeni Zitto, tamaa ya madaraka itakuua! mara hii huwataji tena? ushahidi c ulisema unao sasa tatizo nn?
ReplyDeletewewr zitto mshenzi nini,mbona unakuwa kama bata anayetafuta pa kuharisha,tupishe kiranga tu tumekuchoka
ReplyDeleteMbona huna msimamo kamanda unachange mind kila siku.
ReplyDeletehuyu kijana ni mtu wa sifa sana na tamaa zake za madaraka, alianza vizuri lakini anakoelekea siyo pazuri
ReplyDeleteme ushauri wangu tu kwako Zitto, ungetulia Chadema kuendeleza mapambano kumg'oa huyu fisadi, mbona ungefika mbali tu, kuliko kukaa na kutumiwa, sasa ndiyo unawasaidiaje watanzania hivyo kwa kununuliwa?
ReplyDelete