Katika kipindi cha hivi karibuni, mrembo wa Kenya Lupita Nyong’o ameipeperusha vyema bendera ya nchi yake kwa kuteka vichwa vingi vya habari akiwa anang’aaa katikati ya mastaa wa Hollywood baada ya kufanya vizuri kwenye filamu ya ’12 Years A Slave’ aliyocheza na Brad Pitt na mastaa wengine.
Kwa mujibu wa Jarida la National Inquirer, muigizaji wa kike mwenye mafanikio makubwa ambaye ni mpenzi wa Brad Pitt, Angelina Jolie ameonesha wivu kutokana na mgongano uliooneshwa na Brad Pitt kwa Lupita Nyong’o.
Brad Pitt alimwagia sifa hadharani mrembo huyo wa Kenya kwenye ‘Producers Guild Awards’, na kudai kuwa ni ‘special’ na kwamba wataona vitu vikubwa kutoka kwake.
“She’s very special, a very special young lady. We’re going to see great things from her.” Alisema Brad Pitt kuhusu Lupita Nyong’o.
Baada ya tukio hilo, Brad Pitt alisafiri hadi Australia kuungana na Angelina Jolie na watoto wao sita, ambapo chanzo kimoja kililiambia The Inquirer kuwa Angelina alionesha hali ya kukasirishwa na anachokiona kati ya Brad Pitt na Lupita.
Chanzo hicho kiliongeza kuwa Brad amekuwa akizunguka sehemu mbalimbali duniani na kuonekana kama mtu ambaye hana mke na yuko huru.
“He wasn’t welcomed with open arms. She told him that he didn’t need to make his ‘crush’ on Lupita so obvious to the entire world. Angie is working her tail off, juggling directing duties and caring for their kids. Meanwhile, Brad is running around on the other side of the globe acting like a carefree bachelor.”
Inasemekana kwamba Brad alikuwa karibu sana na Lupita wakati wa Producers Guild Awards na kwamba wakati ambapo Leonardo Dicaprio alipombusu mashavuni Lupita Nyong’o, Brad Pit alimtania, “Hey, man stay away from my girl!”
Bado ukweli wa mambo haujajulikana kwa kuwa kuonesha wivu bila vitendo ni vigumu kuthibitisha!
Source:Times Fm
ANGELINA JOLIE AONYESHA WIVU LIVE BAADA YA MUMEWE BRAD PITT KUWA KARIBU NA LUPITA NYONG'O WA KENYA
8
January 31, 2014
Tags
Huo ni mtizamo wako binafsi
ReplyDeleteBrad Pitt ana penda black .Robin given mke wa Tyson Mnakumbuka Tyson alitaka kumuua Brad .google brad Pitt vs Tyson
Deletewhat goes around comes around
ReplyDeleteSometimes it goes around and away..
ReplyDeleteHuyo Angelina si alimnyang'anya Brad Pit kutoka kwa Jennifer Aniston,mwache na yeye yamrudie!
ReplyDeleteWaume wote wa Angelina kaiba
Deletekina wemw na penny wako pia ulaya.
ReplyDeleteBig up kwa hii story sikama blogs zingine kila kukicha ni Domo na Wema kila siku hata hazina mapya.
ReplyDelete