Habari zilizotufikia sasa hivi kutoka Singida zinasema watu 13 wamefariki dunia baada ya kutokea ajali ya magari mawili kugongana uso kwa uso eneo la Isuna mkoani humo.
Habari zinasema ajali hiyo ilihusisha gari aina ya Toyota Noah na lori ambayo namba zake za usajili hazikupatikana mara moja. Watu 13 waliofariki walikuwa katika Noah iliyokuwa ikitokea Itigi na maiti zao zimehifadhiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Singida.
Baada ya ajali hiyo, dereva wa lori na msaidizi wake walitokomea kusikojulikana.
Mungu awalaze mahala pema amin
ReplyDeleteHiyo noah ilikuwa imebeba watu wote hao? Jamani ajali zinatumaliza
ReplyDeletenataka kujua
ReplyDeletedreva mzima?
Nataka jua gari langu lipo salama?
ReplyDeleteInna lillah wainna illah rajiun
ReplyDeletepoleni mlofiwa wote na majeruhi Mungu awape afya njema
Poleni familia ya marehemu
ReplyDelete