BREAKING NEWS: ASKARI WATANO WAFARIKI DUNIA

Na: Halima Kiondo

Kwa taarifa zilizotufikia HIVI PUNDE. Askari WATANO wafariki papo hapo baada ya bus aina ya Mohamed Trans, kugongana uso kwa uso na gari ndogo aina ya Toyota Corola iliyokuwa ikitokea Dodoma mjini ambayo lilikuwa na sakari hao kisha kupoteza maisha.

Akizungumza na Radio One, Kamanda wa polisi Mkoani Dodoma, David Misime, amesema kuwa ajali hiyo imetokea majira ya saa 9 usiku kuamkia leo katika kijiji cha Namtumba Mkoani Dodoma na abiria waliokuwemo kwenye Bus hilo hakuna aliyejeruhiwa.

"Hakuna aliyejeruhiwa kutoka kwenye Bus hili, lakini Dereva aliyekuwa anaendesha abiria hao anafahamika kwa jina la Juma Mohamed, amekimbia mpaka sasa haijafahamika yuko wapi, ameongeza kuwa gari ndogo aina ya Toyota Corola imeharibika vibaya na baadhi ya miili ya askari hao imeharibika. " Tumeipeleka miili hiyo hospital kwa ajili ya kuihifahi huku tukisubiri mipango ya mazishi," amesema David.

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Inna lillah wa Inna ilayh Raajiun
    (Sisi sote ni wa Allah na kwake tutarejea).

    ReplyDelete
  2. Inna lilah wa inna ilayh rajiun,mabasi ya abiria yameanza tena safari za usiku,ni hatari sana.

    ReplyDelete
  3. bakari kitambulio1 February 2014 at 17:03

    mbona hii habari haijakamilika? Ni askari wa jeshi gani mkuu? Tujuze zaidi

    ReplyDelete
  4. DAH M.MUNGU WAREHEMU NJIA MOJA.

    ReplyDelete
  5. fafanueni habari nyinyi wahandishi hapo ni askari yupi magereza,police,uhamiaji,mgambo au wapi.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad