BREAKING NEWS:MADERAVA WA MALORI TABORA WAFUNGA BARABARA KISA WENZAO WATATU WALIO UAWA

Taarifa iliyotufikia asubuhi hii inasema malori zaidi ya 40 yamezuia njia kufuatia tukio la kutekwa kwa madereva wenzao watatu wa malori na majambazi kisha kukatwa mapanga,na inasemekana baada ya tukio hilo kutokea polisi walichelewa kufika eneo la tukio.
IMG-20140126-WA0003Mbali na malori kuna mabus ya abiria na magari binafsi ambayo nayo hayawezi kupita kufuatia agizo la madereva hao ambalo wamesema hawaachii njia mpaka Mkuu wa Mkoa wa Tabora au Rpc  afike,huku wakidai hilo limekua ni tatizo sugu eneo hilo kutokana na kutokea vitendo vya utekaji mara kwa mara.
IMG-20140126-WA0006Eneo hili linaitwa laziba lipo katikati ya mji wa Laziba na Nzega,ni kilomita 20 kutoka Nzega Mjini,madereva hao wa malori wameziba njia tangu saa 3 asubuhi hii,japo taarifa inasema tukio la kutekwa kwa madereva hao limetokea jana  saa 3 usiku.

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Tunawashukuru sana mgomo wa leo labda utatusaidia maana nzega majanga matupu.

    ReplyDelete
  2. viogozi wenyewe ni majambazi sasa nani atalinda wana incha jamaniii? yaani nchi imekuwa kama haina serikali? toba yarabiii

    ReplyDelete
  3. Funguka hamdani wanatakiwa watuwekee ulinzi mkali sana maeneo haya yanatisha ukipita ushukuru mungu.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad