DR LWAITAMA ALIKUWA SAHIHI KUOMBA PRECISION AIR WATUMIE LUGHA YA KISWAHILI KUMPA MAELEKEZO
12
January 31, 2014
Kwa ufupi maofisa wawili waandamizi wa safari za anga wamesema msafiri halazimishwi kujua lugha inayotumika kwenye ndege bali maafisa wa ndege ndio wenye wajibu wa kuhakikisha mteja wao anapata mawasiliano kwa jinsi atakavyo elewa. Wamesema ikihitajika wanatakiwa watumie hata lugha ya ishara. Wamesema kwa afrika mashariki lazima maafisa wa ndege watumie aidha kiswahili,kiingereza au kifaransa(lugha kuu za ukanda huu)kuwasiliana na wateja wao,na ikishindikana watumie ishara. Kwa issue ya Dr.Lwaitama wamesema kwa kuwa issue ilikuwa ni kuhusu kumuelekeza jinsi ya kufungua mlango wa dharula,mbona kama walishindwa kumwambia kwa swahili ilitakiwa hata kwa ishara wangemuelekeza kuliko kumwambia kama haujui kiingereza hama kiti?.Wame nukuu vipengele kadhaa vya sheria za usafiri wa anga.Source:Power Breakfast Clouds fm.My take:Dr. Yupo sahihi na taasisi nyingi Tanzania bado zinadharau tamaduni zetu na kutukuza ukoloni mamboleo!
Tags
kwa kuwa alikuwa sahihi basi afidiwe kwa kumpotezea muda wake mwingi na hao watumishi wa hiyo ndege wawajibishwe kwa kukurupuka kufanya maamuzi ya kipuuzi pasi kumsikiluza mteja wao.
ReplyDelete-...........,...,. mi napita tu.........,.......
Alikuwa sahihi vipi wakati kila carrier ana utaratibu wakea, hivi ni kweli Dr. Hajui ngeli mbona anakuwaga in todays inperspective.
ReplyDeleteIsijekuwa katumwa kuvuruga biashara ya watu? Waswahili mbona tunayo miongozo yetu kama funika kombe.........
Ila source tatizo !
Bado upo enzi za colonialism
DeleteHakuna lolote, inamaana huyu Dr.haijui lugha ya kiingereza?huyu mzee kwakua amezoea kuchallenge issues kwenye majukwaa ya siasa sasa anataka kuingiza hayo kwenye business za watu.Akitaka kiswahili wkt anasafiri apande mabasi ya mikoani.
ReplyDeletehahaaaa wadau mnafurahisha sana,Dr kingereza anajua tena sana cauz aliwahi kuwa lecturer wangu UDSM anafundisha philosophy ila anapenda kudumisha kiswahili sana
ReplyDeleteYaani John unashangaza sana, utadhani hujawahi kufanya kazi ktk airline bwana! Katika hilo la your take, you are wrong!. Huyu dk alikuwa na makosa kuleta mzaha wakati watu wapo kazini. Ndege imekaribia kupaa kisha unaleta mzaha!!..vipi wakiwa huko angani na wakapata daharura kweli hawezi leta mzahaa? sawa basi mzaha lakini ukishaelezwa sababu unatakiwa utii na utafute wakati na mahali muafaka wa kuleta mapendekezo yako, sio wakati ule ule unaotaka wwe. Tatizo lake alidhani kwa kuwa yeye ni dk na anaonekana sana ktk TV basi kila mtu anamjua. Na hii iwe ni fundisho kwa wote kwamba usilete mzaha na kazi za watu hasa katika suala la usalama. Kama yeye anaona alikuwa sahihi na ameonewa basi akafungue kesi mahakamani kudai fidia tuone kama atashinda!
ReplyDeletepoint ni kwamba ile ndege ipo registered tanzania, how come wasitumie lugha yetu kama media of communication? lazima tutetee utamaduni wetu...
ReplyDeleteUnaweza kuwa sawa kwa point , lakini Dr.alileta maada yake at a wrong time & place . air hostess at that time wanachohitaji ni corporation yako na kuwa na assurance kuwa incase of emergency unajua nini cha kufanya for the sake of other passengers life.
DeleteUkipanda Ndege ya KLM wanatangaza kidach na kingereza,ukipanda Kenya air ways wanaongea Kiswahili na Kingereza,ukipanda Emeret wanatangaza kiarabu na kingereza kwanini wao precision wasitangaze kiswahili na kingereza? Mzarao. Kwao mtumwa Dr uko right!!!!
ReplyDeleteHoja niya msingi lakini, je ilikuwa ni sahihi kwa Dr.kuanzisha timbwili kwa wakati ule?angeweza kupendekeza hoja hiyo ijadiliwe kwenye management.Dr.alikuwa na hoja nzuri but was presented at the wrong time, place and to the wrong person.hivyo he was wrong.
DeleteTatizo watu bado watumwa wa kifikra maana hadi Leo tunajidharau Na kudharau kilicho chetu..Dr uko sahihi
ReplyDeleteAcheni ujinga huyu ni Dr lakini akili za kikoloni, asilete umaarufu kwenye biashara za watu, awe anapanda mabasi mbona mengi
ReplyDelete