DR LWAITAMA ASHUSHWA KWENYE NDEGE YA PRECISION AIR ALIPOHOJI KWANINI ASIPEWE MAELEKEZO KWA LUGHA YA KISWAHILI

Ifuatayo ni nukuu ya taarifa aliyoiandika Ndimara Tegambwage jana Jumapili, Januari 26, 2013...
Dk. Lwaitama atolewa kwenye ndege, akamatwa na polisi Mwanza

Niliongea na Dk. Azaveli Lwaitama akiwa Mwanza baada ya kuandika maelezo yake kwenye kituo cha polisi cha uwanja wa ndege Mwanza na kuachiwa kwa kilichoitwa "dhamana ya polisi." Anatakiwa kuripoti polisi uwanjani hapo kesho asubuhi kuona iwapo polisi wameamua kumfikisha mahakamani. Nasimulia alivyonisimulia.

Dk. Lwaitama alitoka Dar es Salaam leo asubuhi. Akatua Mwanza. Alikuwa anakwenda Bukoba. Alipanda ndege ya kampuni ileile iliyomtoa Dar es Salaam leo hii - PrecisionAir. Hii ya kwenda Bukoba ilikuwa Na. PW 0492. Alikwenda hadi kwenye kiti chake Na. 2B. Hapa ndipo kuna milango ya dharura kwa pande zote mbili za ndege - kulia na kushoto.

Ndipo akaja mfanyakazi wa ndege. Akamuuliza iwapo anajua Kiingereza. Baada ya mzaha wa kawaida katika kuuliza iwapo 
ni lazima kujua Kiingereza, ndipo mfanyakazi akamwambia kuwa kama hajui lugha hiyo basi ahame kiti na kukaa kwingine kwani kuna maelezo rasmi ambayo yanatolewa kwa "lugha ya anga" - Aviation Language.

Ilikuwa katika kujibizana kwa nini lugha ya anga isiwe lugha ambayo abiria wengi wanaelewa - huku Dk. Lwaitama akisema katika ndege nyingi alizosafiri kote duniani alikokwenda, lugha za anga huwa zile za wasafiri wengi wa eneo husika na lugha nyingine za kimataifa; huku akishauri kuwa maelezo yangekuwa kwa Kiswahili na Kiingereza - ndipo mhudumu alikimbilia mwenzake ambaye naye hakutaka kumsikiliza Lwaitama na wote wawili wakakimbilia kwa chumba cha rubani kushitaki kuwa kuna mtu "anafanya fujo." Tayari Dk. Lwaitama akawa abiria "hatari."

Rubani hakutaka kusikiliza abiria wake anasema nini; hakumuuliza hata mwenzake waliokaa pamoja juu ya fujo alizoripotiwa; alimwambia hawezi kusafiri. Akaita polisi ambao pia hawakuuliza lolote juu ya fujo zake bali walifanya kazi moja ya kumtoa nje mkukuku.

Ni rafiki yake aliyemwita Diallo na mwanaharakati Sungusia ambao anasema aliwapigia simu wampelekee mawakili ili aweze kuandika maelezo yake mbele yao. Mawakili walifika na yeye kuadika maelezo. Mizigo yake imepelekwa Bukoba. Yeye amebaki Mwanza na kompyuta yake ndogo ya mkononi.

Dk. Lwaitama anasema, "Sina mgogoro na kampuni ya PrescisionAir, bali wahudumu ambao hawataki hata kupata maoni ya abiria. Kwanza, walipata bahati ya kuona mtu anahiari maoni moja kwa moja. Pili, kama wanafanya kazi kwenye ndege watakuwa wamesafiri katika ndege za wengine ambako niliyokuwa nayasema ni maneno na vitendo vya kawaida. Sasa fujo ni nini katika hili?

Mwalimu huyo mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam anasema, "Hata polisi ni wa kushangaza. Mtu anakwambia huyu kafanya fujo, wewe huulizi ni fujo gani. Unambeba tu mzegamzege. Sidhani kama huu nao ni utendaji bora katika nchi iliyohuru; ambako polisi wanapaswa kuwa na utulivu wa akili na kufanya kazi kwa kufikiri kuliko kwa kuambiwa tu."

Dk. Lwaitana anaamkia kituo cha polisi uwanja wa ndege kesho asubuhi kuambiwa "uamuzi wa polisi."

Haikufahamika iwapo mhudumu wa ndege mswahili, aliyekuwa anaongea Kiswahili, hakuwa na tafsiri ya maneno ya Kiingereza ambayo alitaka kumwambia abiria wake.
Tags

Post a Comment

14 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Katiba ya kaz iheshimiwe usiingize ubosi wako

    ReplyDelete
  2. Huyo mzee hajui kuongea... ongea yake ni kishenzi, dharau na kuamuru. Aliwaboa wahudumu kwa kuwasilisha anachodai maoni kwa ujuwaji badala ya ueledi.

    Hata mijadala yake unaweza kuona kabisa jinsi anavyoweza kukufanya uchukie ukweli kwa jinsi anavyo uwasilisha... AJIFUNDISHE HEKIMA YA KUWASILISHA FIKRA NA MAONI YAKE. Amuangalie Prof SHIVJI tunahitaji wazee wenye hekima, busara na taaluma ya ukufunzi kama Prof ISSA SHIVJI.

    UHAYA NA USOMI NI VITU MBALIMBALI.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Acheni usenge,mshamba mkubwa!!!sa nan kakwambia uspecify uhaya,

      Delete
    2. Nadhani Dr ni mtu mwelewa na anajua aongee nn kwa nani na kwa wakati gani,amekuwa mhadhiri UDSM amefundisha wanafunzi wakorofi na watundu tena anazoefu kwenye falsafa huwezi kubishana naye,,unavyoongea naye anajua kama unachosema ni ukweli au uongo,ninavyomfahamu mm cyo mtu wa fujo.Msimhukumu mtu kwa malengo yenu bali uhalisia wake.

      Delete
  3. Kumbe ni muhaya. Wahaya huwa washamba na malimbukeni na majigambo ya kipumbavu, alafu zama zao zilishaisha miaka hiyooooo, kama elimu siku hizi hata wazaramo ni wasomi.

    ReplyDelete
  4. Sisi watz tumekuwa na kawaida ya kudharau wasomi hatusikilizi maoni wala ushari wao. Yaani wasomi sasa ni watumwa kwa wanasiasa kwa mwendo huu tutachelewa sana kuendelea..

    ReplyDelete
  5. MHUDUMU ALIKOSEA KUMUULIZA MTEJA WAKE KWA KISWAHILI ILIHALI ANAJUA ILE SEHEMU NIYAWAINGEREZA ALITAKIWA AULIZE KWA KINGEREZA ILI KAMA MTEJA WAKE ANGESHI NDWA KUJIBU MASWALI ALIYOMUULIZA KWA KINGEREZA HAPO ANGEJUA KWAMBA HAJUI KINGEREZA WEWE MTEJA AMEKAA SEHEMU YA WATU WANAOJUA KINGEREZA ALAFU UNAULIZA KWA KISWAHILI HAPO INAONYESHA HATA HAO WAHUDUMU KINGEREZA KINAWAPIGA CHENGA PIA ANASTHILI ADHABU KWA KUMBUGUZI ABIRIA

    ReplyDelete
  6. huwezi kumlaumu muhudumu. wahudumu huwa wanaaandikiwa procedure za kuwaeleza abiria kwenye ndege. inaelekea prof alikaa kwenye emergency door ambapo ni lazima uelekezwe namna ya kufungua mlango ikitokea emergency landing. sasa kama maelekezo hayapo kwa Kiswahili muhudumu afanyaje? hilo ni tatizo la uongozi!!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Sawa lakini ujue kwenye ndege wana care sana customer, kama habari zenyewe ni za kweli huyo dada hana kazi,sbb anafukuza wateja

      Delete
  7. Yote haya yanaanzia kwenye uongozi mmbovu! Waziri wa mambo ya ndani ktk awamu hii nsona yumo likizoni. Unyama unaofanyika nchini haswa kutokana na baadhi ya vyombo vya dola kuchukua sheria mkononi, hata sishangai yaliyomkuta Proffesor. Uchaguzi umekaribia tuchague viongozi na sio sura au jina. Nimemaliza

    ReplyDelete
  8. Huyu mzee alichofanya ni kuleta ujuaji na kuingiza malumbano ya siasa kwenye biashara za watu. Kampuni has a right to refuse servive to anyone at anytime.
    kama alikuwa na maoni yake angesubiri wakati na mahali fasaha siokuanzisha issues wakati ndege inataka kuondoka.wahudumu na rubani si wakulauniwa, huwezi jua mental status ya abiria na how far anaweza kuri act once ndege ikiwa angani..

    ReplyDelete
  9. Mimi siyo mhaya lakini namtetea Dr. Lwaitama. Dr. Amefanya vizuri. Hao wahudumu hata kiingereza chao hakieleweki. Watumie lugha zote kiingereza na kiswahili. Hapo kosa ni la uongozi la kuwa na mawazo mgando wasiotaka mabadiliko.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad