GRAMMY:KENDRICK LAMAR AZUNGUMZIA USHINDI WA MACKLEMORE, ATOA USHAURI KWA WAANDAAJI

Baada yakushuhudia tukio la utoaji tuzo za Grammy mwaka huu lililofanyika January 26, ulimwengu wa muziki hasa wa hip hop ulipaza sauti nyingi na minong’ono kuhusu ushindi wa Maclemore & Ryan Lewis hasa kwenye kipengele cha ‘Best Rap Album’, huku mkali wa michano Kendrick Lamar akiondoka mikono mitupu licha ya kuwa katika vipengele saba.

Rapper huyo toka Compton, California ameelezea tukio hilo wakati akifanya mahojiano na mtandao wa XXL wa Marekeni, na kutoa mtazamo wake kuhusu kushindwa na Macklemore katika kipengele cha Best Rap Album.

Ameeleza kuwa kila kitu kinafanyika kwa sababu na kwamba Macklemore alistahili tuzo hiyo kwa kuwa aliihangaikia.

“It’s well deserved; he did what he did, man. He went out there and hustled and grinded. Everything happens for a reason; the universe comes back around, that’s how it go.”

Hata hivyo, Kendrick Lamar hakurithika na ushirikishwaji wa wana hip hop hasa katika kutumbuiza katika jukwaa hilo, ambapo mwaka huu walipata nafasi chache zaidi kuliko muziki mwingine.

Aliwashauri waandaaji wangeupa nafasi utamaduni wa hip hop kama walivyozipa nafasi aina nyingine za muziki, na kuongeza kuwa sio tuzo za Grammy pekee bali iwe hivyo katika tuzo nyingine zote kwa kuwa wao pia ni sehemu ya ulimwengu wa muziki.

Album ya Macklemore & Ryan Lewis ‘The Heist’ ilishinda tuzo ya Album bora ya Rap, na inasemekana kwamba ushindi wao umesababishwa na uungaji mkono wa mapenzi ya jinsia moja, na hivyo kupigiwa kura na watu wengi ambao wanaisapoti sera hiyo.
Source:Times Fm

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad