Kijana asiye na kazi aitwaye Nolesy aliamua kumwoa rafiki yake wa muda mrefu aliyekuwa akifanya kazi katika benki moja mashuhuri.
Nolesy alijitosa katika ndoa licha ya hofu na ushauri mwingi aliopewa na ndugu kuwa ni vibaya kuoa ukiwa huna kazi.
Kila mwezi yule binti alimpa mmewe mshahara wake wote wa 800,000 baada ya kutoa fungu la kumi kwa ajili ya kanisani.
Nolesy yeye alitoa 200,000 na kumpa mkewe kwa ajili ya matumizi binafsi na zilizobaki kijana aliamua atumie kwa matumizi gani. Na hali hiyo ilidumu kwa miaka mitatu mfululizo.
Furaha na amani viliitawala nyumba ile na kwa wanandoa wale pia kwa miaka mitatu pamoja na kuwa marafiki wengi wa yule dada walimfuata na kumwambia huwezi ukawa unalipa bill zote za nyumba na kufanya kazi zote wewe tuu na mmeo kakaa tuu kwa nini msiachane?
Kuna mwezi mmoja kijana yule alitumia zaidi ya 500,000 akizunguka mikoa mbalimbali kwa ajili ya intavyuu za kazi.
Hatimaye kijana alifanikiwa kupata kazi Mbeya katika kampuni ya Green Entertainments na kuwa meneja mkuu huku akipokea mshahara wa milioni tatu na nusu kama kianzio.
Akanunua gari yake ya kwanza mpyaa kwa bei ya shilingi 18M na akampa funguo mkewe na kuendelea kutumia usafiri wa daladala kwa zaidi ya miaka miwili.
Baada ya hapo akanunua gari la pili jipya lenye thamani ya 30M na kumpa mkewe na kulichukua gari la zamani na kulitumia yeye na mpya kumpa mkewe.Miaka michache baadae wakahamia kwenye nyumba yao.
Siku moja mke alikuwa akitafuta dokyumenti zake katika makabrasha mbalimbali pale chumbani kwao, alishangazwa kuona kuna bahasha ndogo imefichwa na ndani kuna picha yake wakati wa harusi na akaona kuna dokyumenti nyingine za manunuzi kiwanja na magari na vyote vikiwa vimeandikwa kwa jina lake kabla ya kuona maandishi yaliyoandikwa:
''MKE WANGU NI KILA KITU KWANGU. ALIKUBALI KUOLEWA NA MIMI NIKIWA SINA KITU, NA SASA NAAMINI HATA NIKIWA NA VITU VYOTE NI VYAKE KWANI MOYO WAKE NI ZAIDI YA KILA KITU KWANGU NA FAMILIA YETU.AISHI MILELE"
Machozi yalimtoka dada yule na alifurahia sana ujumbe ule kabla ya kukumbuka kuwa wiki chache baadae ilikuwa ni kumbukumbu ya miaka yao ya ndoa.
Hivi sasa MUNGU amewabariki na wana watoto wawili wakike na wakiume na wanapendana mara mia zaidi ya mwanzo.
Jamani mapenzi ya kweli yapo mpaka sasa.
Je una uhakika kuwa mapenzi uliyonayo kwa mwenza wako ni sawa au yanaweza kulinganishwa na haya?
Pamoja na vyote lakini kumbuka mnachaguana ili kuishi kwa shida na raha na haijalishi nani ananunua mahitaji ya nyumbani au kulipa bili kwa sasa.........
HAKUNA HALI YA UMASKINI INAYODUMU MILELE
marriage is for richer and poorer. this story has touched me. I love and will love my husband no matter what the situation will be.
ReplyDeleteHUYO NIMKE ALIYETOKA KWA BWANA! KWANZA ALIKUWA MWAMINIFU KWENYE FUNGU LAKUMI,NA ALIKUWA NA HOFU YAKIMUNGU, BWANA AWAZISHIE
ReplyDeleteNdoto za Cinderela, Abunuasi na Alinacha...crap!!!!
ReplyDeleteMay God continue to bless your marriage
ReplyDeletewastara kasema kwasasa yupo taar kuolewa,ila mwanamke anaemtaka awe milionea,tehe tehe teheeee
ReplyDeletendo za wanawake wengi ni kumpata mwanaume mwenye pesa sio anaetafu
ReplyDeleteHuyo c mwanamke labda n malaika
ReplyDeletehuyo mwanaume pia katoka kwa Mungu heee chezea wanaume ngozi ya tako mpe mshahara wako akahonge haki m bora niwe roho mbaya ila kuja kulia machozi ya damu HELL NO
ReplyDeleteMmh.. Hii stori tu..!
ReplyDeleteYaani ukisikia mke au mme mwema hutoka kwa Mungu yaani hiyo ni yenyewe haswaa. "Thats perfect" Nimeipendaje!
ReplyDeleteI believe in love
ReplyDeleteHata sasa bado Kuna really Love in dis world
ReplyDeleteam in real love lyk thoz couple...ucye amin endelea kutoa macho...
ReplyDeleteUkweli wa moyoni mwangu, binafsi nimeguswa sana na hii taarifa. Ni kama hadithi lakini naamini haya bado yanatendeka kwa walio wachache katika dunia ya sasa. Binafsi bado sidhani kwamba niliye naye anaweza kufikia kilele cha MAPENZI yaliyo elezwa baina ya hao wapendanao, ingawa napenda ikiwezekana MUNGU hampe ufahamu uliofichika kama huo ikiwezekana zaidi.
ReplyDelete