HATARI:WANAFUNZI WA KIKE SHULE MOJA BAGAMOYO WANASHIRIKI MAPENZI YA JINSIA MOJA

Shule moja ya sekondari ya wasichana iliyopo wilayani Bagamoyo mkoani Pwani, imelalamikiwa na wanafunzi pamoja na wazazi kuwa mabinti wanajihusisha na vitendo vya ngono vya jinsia moja (usagaji).

Akizungumza na NIPASHE mmoja wa wazazi (jina linahifadhiwa) alisema shule hiyo imepoteza sifa kwa kuwa kuna wimbi kubwa la wanafunzi wanaojihusisha na vitendo hivyo vya usagaji.

Alisema mtoto wake alikuwa ameanza kidato cha kwanza mwaka jana na baada ya kumuandikisha ndipo baadhi ya watu walipomueleza kuwa shule hiyo kwa sasa ina sifa mbaya ya mchezo ‘huo mchafu.’

"Baada ya kuelezwa nikasema nitalifanyia kazi jambo hilo hivi karibuni katika kupekua madaftari ya mwanangu nakutana na kibarua cha mapenzi alichoandikiwa na msichana mwenzake niliumia sana na nilitumia nguvu kumbana bila hivyo asingeniambia," alisema

Alisema ilimbidi amhamishe binti yake na kujiunga na shule moja ya sekondari iliyopo mkoani Tanga kwa ajili ya kuendelea na masomo ya kidato cha pili mwaka huu.

Mzazi huyo alisema anashangazwa ni kwa nini hatua hazichukuliwi wakati suala hilo ni la hatari kwani watoto wao wataharibika kiakili pamoja na kimwili na wanaweza kuambukizana VVU na Ukimwi..

Alisema wakati mwanaye akisoma katika shule hiyo alikuwa akihudhuria vikao vya wazazi mara kwa mara na kwamba kila kikao walikuwa wakifukuzwa wanafunzi kutokana na mwenendo huo.

"Hili tatizo ni kubwa na kufukuzwa kwa mwanafunzi sidhani kuwa wanatatua tatizo nadhani hakuna usimamizi mzuri kwani wangeweza kudhibiti kwa haraka tatizo hilo kabla ya kuwa kubwa," alisema

Pia alisema ndugu yake imembidi amhamishe mwanae na kumtafutia shule nyingine kwa kuhofia binti yake kurubuniwa kwani wanakuwa ni wadogo na hawaelewi chochote, hivyo inaweza kuwa rahisi kudanganywa na kuingia kwenye vitendo hivyo viovu.

Alisema kuwa hata kiwango cha ufaulu kwa sasa shule hiyo imeshuka kutokana na tatizo hilo kwa wanafunzi .

Hata hivyo, NIPASHE ilizungumza na mwanafunzi mmoja ambaye anasoma katika shule hiyo kuhusiana na suala hilo ambapo alikiri kuwepo kwa jambo hilo na kueleza kuwa wanaofanya mchezo huo ni wa kidato cha tano na cha sita.

"Mimi hawajanifanyia ila najua wanaofanya mchezo huo ni wale walioko kidato cha tano na cha sita," alisema Pia kuna baadhi ya wazazi wengine wamekuwa wakilalamikia jambo hilo na kueleza kuwa ndugu zao imewalazimu kuwahamisha watoto wao kutokana na vitendo hivyo vinavyofanyika shuleni hapo
Tags

Post a Comment

13 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Weka jina la hiyo shule hadharani kwa faida ya wote.kuna haja gani ya kulihifadhi jina wakati wameshindwa jukumu la kimsingi la kulinda na kusimamia maadili.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Huna jipya hii picha mbona ya cku nyng zimepita.na MPEKUZI amefulia tuwekee tunataka kutoa maoni au utakosa wateja

      Delete
  2. Jamani huu uandishi wenu kwa kua mnaweza kulipia bundle au? Maneno yooote uliyoandika halafu huweki jina la shule nani anapata ujumbe? Au kila mzazi mwenye mtoto bagamoyo shule yoyote amuamishe mtoto wake. Msonyoooo mnakera hata mtu aliyeishia drsa la 7 hawezi kufanya uandishi huo.

    ReplyDelete
  3. wala msipate shida wadau hiyo shule ni baobab!!! yaani pale ndio wanapozalisha wasagaji nna ushahidi wa nnachokiongea kuna bint namfaham alifukuzwa kwa hyo tabia

    ReplyDelete
  4. Baobab au inaitwa baboon high school?

    ReplyDelete
  5. jaman hawamwogopi hata Mungu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mdau hapo juu huyo Mungu si mpaka wamjue ndio wamuogope kwani kumjua kwenyewe hawamjui

      Delete
  6. waibadilishe nakuifanya ichukue wanafunzi wa jinsia zote itasaidia kwani huduma nyingine zitapatkana miongoni mwao

    ReplyDelete
  7. Duuu!!! majanga

    ReplyDelete
  8. Ni kweli Baobab na kwa kununua mitihani wanafunzi wafauru ni Noumer. Baobab ni kiwanda cha wasagaji. Mbuta Nanga.

    ReplyDelete
  9. NGOJA NIWE MWALIMU NIKAFUNDISHE HAPO

    ReplyDelete
  10. Duu hiv mashoga wapo 2mpeleke michael wa prison break

    ReplyDelete
  11. Wizara husika iko wapi? Kuhusiana na hili kwani naamini kunasheria za kuifanya shule iweze kusimamia maadili..sidhani km nalo hili ni gumu kwa serikali kulifuatilia na kuchukua hatua ikibidi kuifunga shule.hili si gumu km la sembe au...

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad