Web

HAYA NDIYO MAJIBU YA MWIGULU NCHEMBA KWENDA KWA WANAOPONDA UTEUZI WAKE,AWEKA WAZI ELIMU YAKE

Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha, Mwigulu Nchemba, ambaye jana alikuwa miongozi mwa manaibu waziri walioapishwa na Rais Jakaya Kikwete kushika nyadhifa zao amewaambia watu wanaoponda uteuzi wake kuwa hana haja ya kubishana nao kwani hawamjui. 
Katika maelezo yake, Mwigulu alisema anamshukuru Mheshimiwa Rais kwa kumwamini kuwa anaweza kumsaidia katika kusimamaia sera na mipango ya fedha nchini. Watu wasionifahamu wanadai mimi sina viwango vya kufanya kazi hii; naomba wafahamu kuwa mimi ni msomi mwenye shahada ya ya pili ya uchumi na hivi sasa niko katika masomo ya kupata shahada ya uzamivu.

Mwigulu aliendelea kusema “Kabla sijaingia kwenye siasa nilikuwa nafanya kazi katika Benki Kuu ya Tanzania kama mchumi. Ninakwenda Wizara ya Fedha kusimamia mambo manne ambayo ni uadilifu, ushirikiano, jitihada na huduma madhubuti ambazo zitatolewa kwa wakati mwafaka.


Tags

Post a Comment

11 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Tatizo sio elimu.Tatizo ni busara za kiuongozi. Mungu akujaalie mabadiliko ya haraka ili kuupata utulivu unaohitajika katika nafasi hiyo.

    ReplyDelete
  2. Huyu jamaa hafai kua waziri kwanza alitakiwa awe mkata mk..

    ReplyDelete
  3. Elimu ina mchango wake hasa kwenye kuelewa na ku analyze mambo lakini co kila kitu busara pia zinahitajika, kuna ma prof. Wamesahindwa ku deliver, nimekua nikifuatiilia hoja zako bungeni unaonekana huna busara sana na ni mtu wa jaziba, umekua ukipinga wapinzani hata kama wanasema ukweli na sifa mojawapo ya kiongozi ni kukubali kukosolewa, umekua uking'ang'ania hoja zisizo kuwa za msingi kama ya Mbowe, kwakweli ulikua bado haujaiva kuwa naibu waziri tena wizara nyeti kama ya fedha! Sababu nikijaribu kuangalia CV yako hujawai kuwa hata supervisor wa kitengo chochote sasa sijui kama hii nchi imeishiwa watu ama tumekua tukijaribu watu badala ya kuwapa kazi watu tunaojua kuwa wanaweza! Kwa kweli wewe na Nkamia mlikua bado hamstahili sijajua Rais kama alifikilia kwa umakini, nakumbuka Nkamia ambae yeye najua hata hiyo elimu ni tatizo aliwaita watu Mbwa Bungeni, eti anasema haongei na Mbwa anaongea na mwenye Mbwa sasa huyu mtu unampa Wizara, any way bado mwaka mmoja na nusu tufanye uchaguzi najua rais ajae hawezi wapa uwaziri tena. Mungu ibariki Tanzania

    ReplyDelete
  4. Huna lolote bro

    ReplyDelete
  5. mdau 10:25 pm big up

    ReplyDelete
  6. ishia kulee mkishapewa uwaziri kama kina nchimbi mnajisheuaga hivi hivi, mimi msomi mimi vile hakuna kama mimi bla bla kibao maendeleo hakuna. hata chenge aliyesoma harvard the best uni in the world alilifanyia nini taifa la bongo zaidi ya ufisadii? wewe umefurahia ulaji na si kingine kafieni mbele mafisadi wahed!!

    ReplyDelete
  7. hii system ati lazima mtu awe mbunge ndio awe waziri ibadilishwe yaani inakera mnoo manake kuna wasomi wenye phd za uchumi na wanapiga kazi haswa hawa ndiyo wanastahili hivi vyeo wanavyopewa hawa mamburulaaz kisa ati ni wabunge. jamani sasa profesa maji marefu siku akipewa uwaziri sijui itakuwaje. kwa mantiki hii maendeleo bongo bado sana sanaaa mganga wa jadi mbunge? huu ubunge nao waweke vikwazo walau mtu umepiga hadi kidato cha sita manake bungeni kuna watu wako ovyo ovyo tuu bora liende mnakula hela za walipa kodi mbwa sana yani tanzania ni taifa la ajabu sana... naibu IGP hakunaga dunia nzima only in bongo ptuuuuuu

    ReplyDelete
  8. Mdau 10.25 unafaa kuwa waziri!

    ReplyDelete
  9. Ana mwaka mmoja na miezi michache,

    ReplyDelete
  10. Hamna kitu. Hufai

    ReplyDelete
  11. Wamempa umaziri kama kazawadi kwakuwa amekuwa mropokaji mzuri wa chama.ccm haina vjana vichwa sasa dogo akatumia adu antage eti kujifanya mtoto wa mjini basi akaonekana mjanja,chama kina wazee sana na hawataki kutoa chance kwa vjana,sasa nchemba akawa deal,couse ilijitahidi kuwapinga upinzani hata walipokuwa na hoja ya msingi.well hao ndio viongoz tulionao,bt mwisho umefika ,nch hii itapata watu waaminifu na watanzania watafurahia kuwa watanzania

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad