HUYU NDIYE MSANII WA BONGO MOVIE ALIYEJINYONGA GESTI,PICHA,CHANZO NA TAARIFA VIKO HAPA


Marehemu Victor Peter enzi za uhai wake.

MSANII Victor Peter kutoka Bongo Movie amefariki dunia usiku wa jana kuamkia leo 28/01/2014 kwa kujinyonga katika gest moja iliyotambulika kwa jina la SAFARI JUNIOUR ilioko maeneo ya Kisosora huko mkoani Tanga.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya mkoa wa Tanga Bombo,tulipofatilia tukio hilo ilifanikiwa kuongea na mmoja kati ya wasanii walioshirikishwa na marehemu katika filamu yake ya
mwisho kabla ya kujinyonga huku filamu yake ya kwanza ikiwa bado haijatoka na kuingia sokoni yenye jina la CHOZI.

Msanii huyo aliyetambulika kwa jina la usanii Koba aliiambia kwamba siku moja kabla ya tukio Victor alifanya nao Shuting ya filamu iliotambulika kwa jina OUR FAMILY ambayo ilikuwa ndio filamu ya marehemu Vicktor ya pili tangu ajikite katika tasnia ya filamu Bongo Movie,

MSEMAJI

Cha kushangaza ni kwamba filamu hiyo muhusika mkuu alikuwa ni marehemu Vicktor na katika filamu hiyo alicheza kwamba kuna msiba baba yake kafa na yeye mwenyewe mwisho wa filamu Picha yake hiyo mnayoiona hapo juu ilipigwa Ex na muhusika aliyecheza kama mdogo wake, Matokeo yake alivyomaliza kushut aliondoka na wasanii kadhaa wakaelekea katika ATM iliokwepo maeneo ya mjini kutoa hela ili awalipe wasanii walihusika katika kazi yake,

KABLA YA TUKIO

Kwa bahati mbaya ATM machine ikagomagoma kwa tatizo kidogo la kimtandao katika kusubiria mtandao ukae sawa marehemu Vicktor alibadilika na kuonekana kama amechanganyikiwa na kuonekana hayuko sawa, Basi kwa bahati nzuri baada ya mda mchache ATM ilikaa vizuri na yeye mwenyewe ile hali ikatulia akatoa hela wakaelekea Hospitali ya Ngamiani huko mkoani Tanga,
Kufika Ngamiani daktari akatoa tamko kwamba apelekwe Hospitali kuu Bombo. 

UCHUNGUZI

Kufika Bombo akapimwa kila kitu na kukutwa mzima hana tatizo lolote lile ikabidi warudi Gest walikofikia huko maeneo ya Kisosora, Marehemu akawalipa wasanii wote na kuwauliza kuwa kuna mtu anaemdai? Wakamjibu hakuna. Kila msanii akaingia chumbani kwake na kuendelea na zake, Kwa wakati ule marehemu aliingia chumbani kwake na kwakuwa ni Self Contain si rahisi kumuona mtu akitoka nje hovyo hovyo.

TUKIO

Asubuhi yakuamkia jumanne 28/01/2014 Wasanii wenzake walimgongea mlango wakaona kimya wakapatwa na wasiwasi ikabidi wamuite mwenye Gest na kusimulia hali halisi mwenye Gest akachukua jukumu la kwenda kutoa taarifa kwa mwenye kiti wa Serikali za mitaa mwenye kiti akatoa taarifa Polisi, Gari ya Polisi ikatia timu katika eneo la tukio na kuvunja mlango wakakuta mwili wa marehemu Victor ukiwa umening'inia kama unavyoonekana hapo pichani alitumia mkanda wake mwenyewe wa kiunoni kujinyongea. Vicktor kajinyonga na kuiaga dunia.
MWILI WA MAREHEMU


Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali kuu ya mkoa wa Tanga Bombo. Marehemu ni mkazi wa mwanza na ameacha mke na mtoto mmoja, Mpaka sasa baadhi ya ndugu wa marehemu tayari wameshafika na wengine wanatarajiwa kufika kesho wa taratibu za kusafirisha mwili kwa maziko. 'Alisema Koba'
tunawapa  pole ndugu jamaa na marafiki waliofikwa na msiba huo, M/mungu ailaze roho ya marehemu mala pema peponi. R.I.P Vicktor.


Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Shakizi au kiswahili kizuri karogwa! R.i.p

    ReplyDelete
  2. EARN $50 - $100 USD Daily Easy

    http://earnstart.com/?id=145518

    ReplyDelete
  3. mkono wa mtu umehusika hapo.

    ReplyDelete
  4. Wamemuua nini waangalie bank yake

    ReplyDelete
  5. Tuache unafiki Mungu hampokei mtu aliejinyonga mbinguni, na wala hakuna sala ya kumuombea mtu alekwisha fariki kama yeye mwenyewe hakujiombea kabla ya kufa. Sala zooote kabla na baada ya mazishi au mtu kufa hua ni mbwembwe tu hukumu yake hua ipo tayari muda wa kukata roho, hakuna cha rest in peace wala nini. Samahani lakini nimeobgea kidini zaidi kuna watu hawajui hilo mpaka leo. Jiombee kabla hujafa.

    ReplyDelete
  6. Yaah! Sure. Kidini zaidi hakuna binadamu anayeweza kukuombea ukasemehewa dhambi kama ulikufa na dhambi...! Mungu awape wepesi wafiwa hasa wazazi na mke. Sijui kwann kakinyonga. Bado kijana kabisa...!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad