Google adsense ni bidhaa moja wapo ya Google ambayo huwapa chance wamiliki wa blogs na website kujipatia kipato kutokana na matangazo mbali mbali ya makampuni ambayo google huyapokea na kuwapa bloggers kuyaweka kwenye blogs/website zao na mwisho wa siku una pata commision kutoka na idadi ya watu waliotembelea blog/Website yako na walio click matangazo ...
Nimeona niongelee hii issue kutokana jinsi baadhi ya bloggers wanavyolalamika kwani kila wakijaribu kujiunga baada ya muda wanafungiwa account kwa kukiuka masharti ya google adsense...Baadhi ya blogger ambao niliwasaidia kutengeneza google adsense nao pia kuna walio fungiwa na kurudi kwangu wakitaka niwatengnezee nyingine huwa naona huruma sana as ni pesa inahusika tena na unakuta ni blogger mchanga
Kwa kifupi hawa jamaa wana masharti mengi kidogo na ukiyakiuka wanakutumia message kama hii hapa chini :
"Hello,
With our advertising programs, we strive to create an online ecosystem that benefits publishers, advertisers and users. For this reason, we sometimes have to take action against accounts that demonstrate behavior toward users or advertisers that may negatively impact how the ecosystem is perceived. In your case, we have detected invalid activity in your AdSense account and it has been disabled"
Hapo ndio unakuwa umefungiwa hata kama ulikuwa na balance ambayo ulikuwa unategemea utumiwe mwisho wa mwezi ndio basi tena Google wanairudisha kwa advertisers...
Sasa kuna kuna Masharti mengi lakini mimi nitaongelea matatu tu ambayo naweza sema ndio wengi hufungiwa account zao kwa ajili hiyo ....
1. Don't click on your own Google ads (Usibonyeze Matangazo ya google wewe mwenyewe kwenye blog yako)
Hilo ni Tatizo hasa kwa bloggers wachanga huwa wanataka kujaribu kila kitu wakishakuwa na blog ...So wakishakuwa na google adsense wanajaribu kuclick yale matangazo waone nini kitatokea ama tu kwa kutaka kujiongezea hela....Ila jua kwamba google adsense wameweka robots za ambazo zinaangalia IP adresses , wewe kama Admin ukitumia hiyo Computer yako kubonyeza matangazo wanajua ni wewe unajitafutia hela so at the end of the day watakufungia ....Watu wanaohitajiwa kuclick ni visitors wengine sio wewe mwenye blog...
2.Impressions (Sijui kiswahili chake vizuri ila hii ni ile wewe as admin kufungua fungua au kuview blog yako wewe mwenyewe mara kwa mara)
Kwa uzoefu wangu naweza sema hili ndio tatizo kubwa linalofanya Google adsense account nyingi kufungwa, hili tatizo ukisoma kwenye policy zao hawajalielezea vizuri lakini limewaumiza wengi sana nikiwemo mimi , mimi kabla sijajua nimeshawahi kufungiwa account mbili mwaka 2010 lakini nilipata solution mpaka leo naenjoy Google money.
Napenda kusema kuwa ukishakuwa na google adsense kwenye Blog/Webiste yako unatakiwa uwe mpole..kazi yako iwe kupost tu, kuview ulichopost achia visitors....Wengi tuna tabia ukishapost habari unaifungua na wewe kuangalia imekaaje hii inasend invalid impression to google kwasababu kila impression au mtu anapoview blog kuna hela inaingia kwenye account yako ya Google so ukiwa unafungua wewe mwenye mara kwa mara Robots zao zinaona kama unacheat na kujitafutia hela mwenyewe...So basi angalau view blog yako mara moja kwa siku ukiangalia mara kwa mara unajiweka katika hatari ya kufungiwa.....
Kama utashindwa hilo la kuview blog yako basi weka ADBLOCKER kwenye Browser yako unayotumia kuview blog ..Adblocker ni extension katika brower inayozuia matangazo kuonekana..Ukiwa umeinstall Adblocker Kwenye Browser yako Matangazo ya Google yanafichwa so itakusaidia...Mimi nimefanya hivyo ....
3. Adult Content,
Hii nadhani inaeleweka tu , hii naweza sema hutakiwa kupost mambo ya ngono ngono sana ...iwe picha ama maneno makali ..(Katika hili tuna advantage moja kwa lugha ya kiswahili bado hawajaweka maneno mengi ya kiswahili katika Robots zao Ila wale wakizungu wanaipata fresh....
Mwisho napenda kusema Google Adsense ni njia nzuri sana ya kujipatia kipata bila longo longo as longer as una visitors wengi kwenye blog yako
--------------------------
John Kiandika
JINSI YA KUFANYA ILI USIFUNGIWE ACCOUNT YA GOOGLE ADSENSE KWENYE BLOG/WEBSITE YAKO
10
January 29, 2014
Tags
asante sana mr admin umetufungua macho tulikua hatujui tunachokifanya......God bless you
ReplyDeleteNimesoma maelezo yako ss nitakupata wapi ili niweze kujiunga au kupata maelezo mazuri toka kwako na mm nikanufaika
ReplyDeletehaya ndo mambo ya kupeana habari co jr na lulu cjui pumbu za diamond zimefanyaje wacha 2jifunze kula pesa na sisi
ReplyDeleteAdmin nashukuru kwa kunifungua,mimi mpaka sasa nimefungiwa account kama tatu hivi ,mpaka nakata tamaa sasa.
ReplyDeletenashukuru sana kwa msada wako
ReplyDeleteasante
ReplyDeletenakubali sana brother, wengi wetu tulikuwa hatujui- tunashukuru kwa msaada wako - ila fanya kama unatuachia namba za simu
ReplyDeletenakubali sana brother, wengi wetu tulikuwa hatujui- tunashukuru kwa msaada wako - ila fanya kama unatuachia namba za simu
ReplyDelete> Got u Brodah!
ReplyDeleteDah bro mm Google AdSense wamenitia text dah wal siiyelewi
ReplyDelete