Naibu Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia (pichani), amewaomba wadau wa habari kushirikiana naye katika kujenga na kuiboresha tasnia ya habari. Alisema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati akikabidhiwa ofisi rasmi baada ya kuteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kushika wadhifa huo. “Kwa sasa nimekabidhiwa ofisi ili nipiganie haki na maslahi ya wanahabari na siyo kama watu wanavyofikiria kwamba nimekuja kudidimiza sekta ya habari,” alisema Nkamia.
Aliongeza: “Mimi nimekuwa mwandishi wa muda mrefu na mwanamichezo. Najua changamoto zilizopo katika tasnia ya habari. Kwa hiyo, ndugu zangu waandishi tushirikiane pamoja ili tuweze kutatua matatizo yanayoikabili tasnia hii ya habari kwa jumla.”
Nkamia amekuwa mmoja wa wabunge waliokuwa wakiwabeza wanahabari katika vikao vya Bunge mjini Dodoma.
Miongoni mwa kauli alizowahi kuzitoa zilizoonekana kuwa ni za kukebehi tasnia ya habari, ni ile aliyohoji kama Baraza la Habari Tanzania (MCT) na Jukwaa la Wahariri (TEF) ni NGO’s (mashirika yasiyokuwa ya kiserikali) au taasisi ya serikali kiasi cha kutoa tamko na nyingine kuwaita waandishi wengi Watanzania kuwa ni makanjanja.
CHANZO: NIPASHE
JUMA NKAMIA AWAANGUKIA WADAU WA HABARI...AOMBA USHIRIKIANO KAULI ZAKE ZAMPONZA
6
January 22, 2014
Tags
KIKWETE NAE WAKATI MWINGINE SIJUI ANAFIKIRIA NINI,YAANI WASOMI KIBAO WALIOJAA HAPA BONGO YAANI KAONA AMPE UONGOZI HUYO KILAZA,SIJUI SERIKALI YETU HII INAELEKEA WAPI?
ReplyDeleteMi siamini kwali Tanzania tumeishiwa watu kiasi hichi? Kweli hichi kipengele cha waziri lazima awe mbunge kibadilishwe haraka hata kabla ya katiba mpya, huyu bwana bado kabisa kuwa waziri, hana uzoefu wa uwongozi wowote, alimu ndio hiyo ana diploma sijui ya nini kwanza naye kanjanja tu hana busara nakumbuka siku moja alisema bungeni eti anaongea na mwenye mbwa sio mbwa akiwakashifu wabunge wa upinzani, sijajua rais amefikilia nn du kweli nchi haina watu
ReplyDeleteNatamani kufahamu je ni vigezo gani anavyotumia rais kuchagua mawaziri. Maana baadhi ya viongozi ni makanhanja. Hivi hawa mawaziri waliochaguliwa ni hawahawa mabingwa wa matusi bungeni wengine. Ngamia anaewaita wapinzani mbwa na kuwadharau wanahabari wezie. Hali kadhalika nchemba ndo bingwa wa kuropoka. Kama vigezo ni kuropoka bungeni sawa, lkn kama kunasifa nyingine hapo mkuu kapoteza.
ReplyDeleteKUONGOZA WIZARA NAKO KUNATAKA HEKIMA YA HALI YA JUU SANA PIA NA KIWANGO CHA ELIMU KILINGANE NA NAFASI YA MTU HUYO, KWANI KAULI CHAFU BILA KUTUMIA HEKIMA HIYO TAYARI INAWEZA KUMUANGUSHA KATIKA KUTEULIWA KWAKE HAPO RAIS APACHUNGUZE SANA. NDIO MAPUNGUFU YAPO KWA KILA BINADAMU LAKINI HATA IKIBIDI YAPIMWE KWA KWELI KUCHAGUA KIONGOZI AMBAYE SIFA ZAKE ZA KWANZA KATIKA KUJIPIMA TAYARI ZINAONYESHA KUWAKATISHA TAMAA WANANCHI HUYO UJUE HAFAI
ReplyDeleteRAIS MWENYEWE NI KILAZA VILEVILE, NDIO MAANA ANATEUA VILAZA WENZAKE.
ReplyDeleteMTU ANAETUKANA HADHARAN SI MWADILIFU NI MUHUNI, HAFAI KUWA KIONGOZI, JK HAZINGATII UADILIFU KTK UTEUZI ILA USWAHIBA NA UJAMAA, HUWEZI KUMPA UONGOZI MTU ANAYEINGIA MJENGONI NA MATINGITINGI YA POMBE!
ReplyDelete