RAIS wa Rwanda, Paul Kagame amenusurika kifo baada ya msafara wake nchini Kenya kupata ajali na kusababisha watu wawili kujeruhiwa vibaya. Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Shirika la Habari la Uingereza (BBC), imeelezwa kuwa ajali hiyo ilihusisha mojawapo ya magari ya msafara wake nchini Kenya, alipokuwa kwenye ziara za kikazi.
Hata hivyo, Rais Kagame hakujeruhiwa katika ajali hiyo iliyotokea saa mbili asubuhi jana eneo la Limuru nchini Kenya. Dereva wa gari hilo alipoteza mwelekeo katika barabara kuu ya Nairobi-Limuru, hata hivyo gari hilo lilikuwa mbali na msafara wa rais huyo. Aidha majeruhi wa ajali hiyo walikimbizwa haraka hospitalini.
Rais Kagame alikuwa anarejea mjini Nairobi kutoka katika kongamano la Magavana wa Kenya mjini Naivasha katika Bonde la Ufa.
Kagame alialikwa kuhudhuria kongamano la Magavana nchini Kenya, kuhusu uongozi mzuri na utawala bora.
Bora engelikufa tu hatuna faida nae ss wa Tz
ReplyDeletejaman 2we na utu
Deletesasa hapo amenusurika vipi kufa wakati gari lake lilkuwa mbali na tukio? vipi nyie waandishi wa siku hizi, habari zenu hazina malengo wala mwelekeo.
ReplyDeletepolen
ReplyDeleteAfe tu
ReplyDeleteunayesema we utaenda wapi achani kutoa hukumu kwa wenzenu anayejua kuketi na kuondoka kwa binadamu nio mungu pekee hivyo mie namtakia long live my beloved prezidar
ReplyDelete