KASHFA YA UZINZI..LISSU AMSAFISHA MBOWE

KATIKA kile kinachoonekana kama kumsafisha Mwenyekiti wa Taifa wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe dhidi ya kashfa ya uzinzi inayomuandama.

Mwanasheria Mkuu wa chama hicho, Tindu Lissu amesema suala hilo ni maisha binafsi ya mtu, ambayo hayawezi kuhusishwa na wadhifa wake kwa namna yoyote.

Akizungumza katika mahojiano maalum ndani ya chumba cha habari cha Global Publishers Ltd, Bamaga, Mwenge jijini Dar es Salaam juzi, Lissu alisema kwa kadiri anavyofahamu, suala hilo ni binafsi linalopaswa kuachwa chumbani, kwa sababu kama litahusishwa na nafasi yake, ni sawa na kukubali kuwa mzee Nelson Mandela wa Afrika Kusini si lolote wala chochote.

“Maisha ya kimapenzi ya mzee Mandela yalikuwa ya ukakasi, kwa maana hiyo unataka tuseme kuwa kwa sababu hiyo, mzee huyu hakuwa kiongozi bora, unataka tuseme Bill Clinton wa Marekani hakuwa kiongozi bora kwa sababu tu alipata kashfa katika moja ya makorido ya Ikulu ya White House? Mimi nadhani haya mambo kama yapo au hayapo, hayahusiani na uwezo wa mtu kiuongozi, ni mambo ya chumbani yanayopaswa kuachwa huko,” alisema Lissu.

Lissu alikuwa akirejea baadhi ya sababu zilizosababisha mgogoro kati ya chama chake na Naibu Katibu Mkuu wao aliyetimuliwa, Zitto Kabwe, anayedaiwa kushiriki kuandaa waraka wenye nia ovu, ambao pamoja na mambo mengine, ulitaka kufanyika kwa mabadiliko ya viongozi wa juu, akiwemo Mwenyekiti wa Taifa, kwa kudaiwa kuwa na elimu ndogo pamoja na kukosa uaminifu katika ndoa yake.

Aidha, hivi karibuni wakati wa kikao kilichomalizika cha Bunge mjini Dodoma, Freeman Mbowe alidaiwa kuvuruga ziara ya mbunge mmoja mwanamke (wa viti maalum) wa chama chake aliyekuwa katika ziara ya kibunge nje ya nchi, na badala yake kumtaka kuungana sehemu alipokuwepo.

Mbunge huyo wa Singida Mashariki, licha ya kukiri kuwepo kwa mgogoro unaokitikisa chama chao, lakini alisema hatimaye Chadema itashinda na kubakia imara na akasisitiza kuwa mwavuli wa mahakama alionao Zito ukiondoka, watamtimua. 

Chanzo: http://www.globalpublishers.info
Tags

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Unajua lisu usifikiri watu wote wajinga unatoa mfano wa uongo na upuuzi mandela ni mke alimkataa akaoa mke mwingine kihalali tena kisheria unafananishaje na mbowe au na yeye wameachana ndio kaamuoa huyo mbunge cliton alifanya kweli na alikili na kuomba msamaha hadharani mmpaaka leo hatujasikia kashfa yake tunataka na mbowe aseme maana yeye ni kioo mbona kila kukicha wasanii wanaandikwa na watu wanasapoti magazeti kua yako sawa kwani wao nikio iweje kwakiongozi mkubwa kama mbowe asiambiwe aache tabia mbaya. kiria kasema kweli mbowe ni muhuni uzuri wa kiria mumewake ni kiongozi na mtu wa karibu na mbowe na yeye ni chadema damu nampa hongera kwakua mkweli ila ashhukuru kwakua yeye ni mchaga angekua muha aangekiona

    ReplyDelete
  2. my friend those are personal issues, u are the once who discuss people instead of working hard for your life.

    ReplyDelete
  3. sasa kama ume2mia kweli
    pesa ya wananch usiambiwe? Alah!

    ReplyDelete
  4. Jaman kam kiongoz akifanya kitu ambacho ni kinyume na maadil ya kitanzania ni lazima wananchi tulioguswa na baya hilo tujaribu kutafuta ufafanuzi wa kina coz c wote waliobahatika kupata elimu ya ujuzi wa mambo pliz wapendwa tusiwe tunajaribu kuugeuza ukweli kuwa uwongo kwa itikadi ya chama fulani au imani ya dini fulani.

    ReplyDelete
  5. We Lissu na mbowe wote matapeli Hanna mwenye sifa ya uongozi hata mmoja

    ReplyDelete
  6. basi tuseme wewe mdau wa jan 17th 3:06 PM ndiyo unafaa kuwa kiongozi, jitokeze bac tukujue halaf tukuchambue tuone kama wewe ni safi!!!! kama hatujakuta matapishi!!!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad