KAULI YA ZITTO KABWE BAADA YA MAHAKAMA KUMPA USHINDI DHIDI YA CHADEMA

Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe jana alitinga  mahakama kuu  kupinga kujadiliwa kwenye kikao cha kamati kuu ya Chadema,Kikao ambacho kilikuwa kikutane leo.

Hii  ni  kauli  yake  baada  ya  mahakama  kumpa  ushindi;
"Jana tulikwenda mahakamani kwa ajili ya jambo moja tu kutaka haki itendeke kwa sababu mahakaama ndiyo chombo cha juu kabisa kwenye nchi yetu cha kuweza kutenda haki mara baada ya kamati kuu ya chama changu kufanya maamuzi ya  kunivua nafasi zangu ambayo niliandikiwa makosa 11

"Nilikata rufaa kwenye baraza kuu la chama ili baraza kuu liweze kuona kama kamati kuu ilifuata taratibu za chama kufikia maamuzi yale japo mimi naamini haijafuata taratibu za chama lakini kwa bahati mbaya viongozi wangu wa chama changu wameamua kuendelea na kikao cha kamati kuu.

"Hawajajibu barua yangu ya nia ya kukata rufaa na kuweza kupatiwa taarifa na mwenendo wa kikao ili niweze kukata rufaa kwa mujibu wa chama. Kwa hiyo nimekwenda mahakani ili mahakama iweze kutoa maamuzi ya mimi kuweza kupata nafasi ya kusikilizwa na kujadiliwa.

"Nashukuru Jaji John Utamwa ametoa amri ya muda ya kuzuia kamati kuu ya chama kunijadili mpaka hapo Chadema watakapoweza kujibu hoja zilizotolewa na mwanasheria wangu Albert Msando.

"Leo tunarudi mahakamani kwa ajili ya kuendelea na kuweza kupokea majibu kutoka Chadema lakini kikao cha leo kamati kuu imezuiliwa na mahakama kujadili hoja yoyote inayonihusu,lakini pia mapingamizi yote mwanasheria wa Chadema Tundu Lissu aliyokua ameyaweka dhidi ya mwanasheria wangu Jaji ameyatupilia mbali kwa hiyo kesi inaendelea.

"Muhimu katika hili ni haki na mimi kama mtu ambaye siku zote natetea haki sasa ni fursa yangu kutetea haki yangu mwenyewe ya kuweza kusikilizwa  ya kutumia taratibu zote za chama katika hali ya kawaida baraza kuu la chama liitwe kwanza  lijadili jambo hili kabla ya kikao cha kamati kuu kuitwa".
Tags

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. zito hatukuelewi, wewe ni mkombozi au ni ccm?

    ReplyDelete
  2. ZITO MNAFIKI HUYOOO! KWENYE JIMBO LAKE ANAMADIWAN 3,WA CHADEMA! SASA2NAJIULIZA ZITO NI CHADEMA AU NICCM?

    ReplyDelete
    Replies
    1. mdau madiwa hupita kwa kura za wananchi sasa ulitaka zito awapigie kura pekeake had washinde?mbona mnavichwa vya panzi,...

      Delete
  3. Mtu yoyote anayepiganiya democrasia huitwa mnafiki badala ya mkombozi@zitto usiogope wala usirudi nyuma watanzania wako pamoja na ww!!!

    ReplyDelete
  4. NAkukubAli sanaa jembe langu Zitto. Usogope tuko pamoja sana.

    ReplyDelete
  5. all in all Zitto ni mpambanaji..hamtaweza kumupelekesha kama mnavyowapelekesha walalahoi wengine..........

    ReplyDelete
  6. Zitto ww ndiye unae takiwa kuchukuwa nafac ya Baba Nyerere tuna kukubali

    ReplyDelete
  7. NABII HAKUBALIKI KWAO........Zitto wewe ni jembe

    ReplyDelete
  8. ukifatilia historia ya viongozi wengi wazuri utagundua kuwa walipitia katika pingamizi kibao na vikwao vingi,zito usirud nyuma tunaokuelewa unachofanya tupo nyuma yako,nipo taar kufunga na kuomba kwaajir yako

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad