KIGOGO WA WEMA NOMA SANA..AMNASA RAFIKI WA WEMA KULIPA KISASI

Tatoo ya Clement Mgongoni Mwa Naima
Stori: Imelda Mtema
NOMA sana! Baada ya kupigwa cha mbavu (kuachwa) na Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu huku akimnyang’anya vitu vyote vya ofisini, yule kigogo wa ikulu, Clement a.k.a CK, hivi sasa anadaiwa kutoka na shosti wa staa huyo, Naima Shaa.

Kwa mujibu wa chanzo makini cha gazeti namba moja la burudani Bongo, Ijumaa Wikienda, Naima anatamba na kuwapiga vijembe wasichana wa mjini kuwa anatoka na CK mwenye mkwanja mrefu (bado fedha hazijaisha).

“Nakwambia hatunywi maji, mtoto kadata kabisa hadi ameamua kujichora ‘tatuu’ ya jina la Clement  kwenye bega lake la kulia. Inahusu?” kilihoji chanzo chetu.

NI MTOTO WA MBUNGE
Mpashaji huyo alizidi kuweka wazi kuwa Naima ambaye ni mtoto wa Mbunge wa Mafia, Abdulkarim Shaa (CCM) hivi sasa anaonekana na mdogo wa CK huku wakiitana shemeji wa ukweli.

“Sasa hivi jamaa anajilia vyake mdogomdogo kwa mtoto Naima pale kati, naona ameamua kumalizia machungu ya Wema kwa Naima.

“Unaambiwa nyuma ya pazia stori ni kwamba anataka Wema aumie ndiyo maana ameamua kubanjuka na Naima huku akijua kabisa kuwa ni marafiki.

“Unajua kama mtu akikuumiza kimapenzi, ukitembea na rafiki yake naye anaumia vibaya mno. Kwani hukumbuki ilivyokuwa kwa Penny (Penniel Mungilwa) alipochukuliwa na Diamond (Nasibu Abdul)? Ilikuwa ni ili kumuumiza Wema na kweli walifanikiwa. Ndicho anachokifanya CK,” kilitiririka chanzo hicho.

WATU WAMEDATA
Chanzo hicho kiliweka wazi kuwa Naima ambaye mara nyingi haoni soni kuonesha tatuu ya jina la Clement, amekuwa akijinadi kuwa yeye ndiye mrithi halali wa Wema na kwa sasa kigogo huyo haoni wala hasikii kwake.

“Naima naye amedata kabisa na sidhani kama anaogopa Wema kujua kama yeye ndiye hasa anatembea na kigogo huyo kwa kipindi hiki,” kilisema chanzo hicho.

UNATAKA KUMSIKIA NAIMA?
Baada ya kupata taarifa hizo, gazeti hili lilimtafuta Naima ili kuthibitisha madai hayo ambapo alikiri kumfahamu CK lakini akadai watu wanamsingizia.

Alipoulizwa kuhusu  tatuu aliyochora yenye jina la Clement, Naima alisema ameandika ‘Element’ na siyo ‘Clement’ (tazama picha, akili ya kuambiwa changanya na yako).

“Yeleuuuwi...jamani watu wananisingizia. Hii tatuu niliyochora nimandika jina Element na siyo Element (angalia maneno yanafafa! Moja alikuwa anamaanisha Clement),” alisema Naima na kukata simu.

WEMA ANAJUA CHOCHOTE?
Baada ya kuwasiliana na Wema kwa njia simu na kumuuliza kuhusiana na madai ya zilipendwa wake kulipiza kisasi kwa rafiki yake, Naima, alisema kuwa habari hizo ameshazisikia lakini anasikitika kwa kuwa kigogo huyo karuka majivu na kwenda kukanyaga moto.

Alisema kuwa ishu hiyo haimuumizi na zaidi sana anawaombea wawili hao maisha mema ya kimapenzi ilimradi moyo wake umeshatua kwa umpendaye.

“Moyo wangu ulishatulia kwa nimpendaye, nawatakia maisha mema,” alisema Wema.

NYUMA YA PAZIA
Uchunguzi wa gazeti ulibaini kuwa nyuma ya pazia la habari hii kuna mambo mengi ya namna CK na Naima walivyokutana.

“Ni Kinondoni pale Mwanamboka. Mke wa CK alikuwa na baa pale ambayo siku hizi imefungwa.
“Naima alikuwa ni mke wa mtoto wa Mwanamboka. Walikuwa wanakutana pale baa. Ndipo mambo yalikoanzia.

“Unajua hata Naima ameingia kwenye gogoro la kindoa na mumewe kwa muda mrefu. Kisa ni huyo CK. Ona sasa wote wamekosa ndoa. Sinema inaendelea,” kilimalizia chanzo chetu. 

Chanzo:Global Publishers

Post a Comment

11 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kwani huyu Clement anamatatizo gani.Huyu ni mtu mzima sana kujihusisha na deal km hizi especially katika public.Ukisikia tenager anahangaika na mademu hushangai but... demn...man
    respect yourself and your family.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mume wa mtu .kweli marriage is a scam

      Delete
  2. Huyo wema ana lolote hapo roho inamuuma kuliko et anasema kafika kwa anaye mpenda anakupenda nani kakwambia sukari ya warembo ana kulove! Ata ulivyoachwa mwanzo na sukari ulisema maneno hayohayo, we daimond anakupenda kwa dawa kutwa na mama yako kwa waganga kumroga daimond tena kwenu wanaume wote waliooa mmewaroga nani ajui na huyo daimond cku akiri itamrudi na ndio mana akikuacha ni mara moja na kashfa nyingi msenge wee mwache Naima afaidi.

    ReplyDelete
    Replies
    1. This shows how miserable ur life is. Ur a big fool hu think mpaka utaje waganga kama ur family wanaenda usione ni family zote. I don't c anything wrong kwa wema kusema amempata am pendaye ka ww hujapata mtu pray to God an get 1. Wema ndio amemwacha Clement na kana yupo na naimah. She should be ashamed of haself mtu alitembea na ur friend wamefanya madudu yote. Ama kweli wabongo mwatia kinyaa

      Delete
  3. Umeonaee mdau! Kwanini daimond anavyojua waganga asilipeperushe ilo liwema manaa kazidi! Linapenda kutobwa na akienda kufirwa cku iyo kama akipewa laki anaiba simu ya mteja wake

    ReplyDelete
  4. Natamani sana kuwa na mwanamke kama wema lakini naogopa sana ukimwi sijui nawezaje kufumba macho nikatafuna tu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Pesa unayo au unatamani vya bure

      Delete
  5. JAMANI MTOTO WA MBUNGE!!!!!
    INABIDI SASA HUYO CLEMENT AFUNGULIWE MASHTAKA KWANI AMEZIDI KUZALILISHA WATU MTU MZIMA MWENYE NDOA ANAFANYA MAMBO AMBAYO HAFANANI NAYO KAZI NIKUTUHARIBIA MABINTI KWAKATI HATAWAOA NA HUYU NAIMA ANAZALILISHA WAZAZI WAKE HUYO SIO MUME ILA NIMCHAFUZI WA WATOTO TENA ANAPEPO WANGONO MTU MZIMA OVYOOOO ETI ANAFANYA IKULU SIJUI HUYU RAIS KAMA ANAYAFAHAMU HAYA KWANI HUO NIUTOVU WANIDHALI NDANI YA OFISI YA IKULU MTAFANYAJE KAZI NA FUSUKA KIASI HICHO INAPASWA AHAMISHWE APELEKWE WIZARA YA UTALII ILI AKAHANGAIKIE HUKO KWENYE MAHOTELI KULE KUNA MACHANGU KUTAMFAA WEMA WALA MSHIPA USIKUUME BURE ILA MUONEE HURUMA RAFIKI YAKO HUYO KUINGIA KWENYE NDOA YA MTU NIHATARI SANA

    ReplyDelete
  6. Kwani na hao mabinti hawaoni au wamelazimishwa naima alishaolewa so hana utoto hebu tuondolee ushuzi wako we hapo juu mnaongea mtasema mmekatwa vichwa.naima mwaya jilie vyako mjini mipango ukimwi upo na unaua zingatia kuwa makini mamii.huyo wema wenu wakati anatembea na mume wa mtu hamkuona mpaka leo kaumbuliwa na CK, na huyo domo wala hampendi kwa dhati asingekuwa anakwenda kwa wanawake afu anarudi kwa bwege lake wema.katembea na Jokate karudi na penny karudi sasa huyo wema si taahira na kama hamjui kilichomrudisha domo kwa wema kashajua mwaka umegeuka anataka kuuza hiyo filamu yake mana anajua domo wema ndo anayempaisha, ndo maana mamaake wema hamtaki domo coz hakuna mzazi anayekataa mume mwema ila kashaona domo hampendi mwanae anamtumia kibiashara na kazi zake.na mama domo hampendi wema coz kaona hafai kuwa mke anapenda sifa za kijinga tangu amekuwa na Endless fame hakuna cha maana alichokifanya ni ushuzi mtupu kamchukua msanii nigeria Omotola mpaka leo hamna lolote misifa tu wenye akili zao wanamcheka huyo boss wenu na nyie team ushuzi nyokonyoko muelimisheni huyo team kujichubua wenu.najua mkiona hii msg mtaporomosha mitusi kama kawaida yenu huko Instagram mmejaza ushuzi wenu tu hakuna tusi jipya tukaneni ila msg imewafikiwa nyauba nyie.sina team yoyote ila ukweli ndo huo mkiweza kama imewauma kunyweni juisi ya tindikali hamna tusi jipya yale yale pyeeeeeeeeeeeeee woote team ushuzi pamoja na huyo Dougimavi wenu na matikimkojo mitege kama banda la kasuku mbayaaa kichwa ka boksi manina zenu

    ReplyDelete
  7. mimi ninavyomuelewa Naima ni mke halali wa SAAD SALIM MWANAMBOKA hawajaachana wana mtoto mmoja,ila kuna matatizo kidogo kwenye ndoa yao

    ReplyDelete
  8. kula maisha clement

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad