LOWASSA ATANGAZA NIA KIMTINDO


Monduli. Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa ametangaza kuanza rasmi kwa safari aliyoiita ya matumaini ya ndoto zake, ambayo amesema itatimiza ndoto za Watanzania za kupata elimu bure, maji safi na maendeleo ya uhakika.

Akizungumza katika ibada ya shukrani na kuupokea mwaka mpya, katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),Usharika ya Monduli Mjini, Lowassa bila ya kutaja safari hiyo ni ipi, aliwashukuru watu wote kutoka maeneo mbalimbali nchini, ambao walimsindikiza katika ibada hiyo.

Lowassa alisema anaamini watu hao waliofika, wana uhakika wa ushindi katika safari hiyo kwa kumtegemea Mungu.

“Nimefarijika sana leo kuwaona hapa marafiki zangu wengi. Ninapowatazama hadi machozi yananitoka na kwa uwezo wa Mungu tutashinda kwani nyote mnajua nia na ndoto yangu,’’ alisema Lowassa na kupokelewa na sauti za shangwe kanisani.

Licha ya kutoweka bayana, Lowassa amekuwa akitajwa kuwa ni mmoja wa wanasiasa wanaowania kumrithi Rais Jakaya Kikwete baada ya kumaliza kipindi chake cha uongozi mwakani.

Azungumzia Katiba Mpya.

Akizungumzia Katiba Mpya, ambayo mchakato wake sasa unaelekea katika Bunge Maalumu, licha ya kuipongeza Tume ya Mabadiliko ya Katiba chini ya Mwenyekiti wake, Jaji Joseph Warioba alisema ana wasiwasi juu ya muundo wa Serikali Tatu.

“Nina wasiwasi na huu muundo, ni vyema viongozi wa dini, kuliombea taifa tupate Katiba bora kwani maoni ya watu asilimia 40 ambao hawakutaka muundo wa Serikali Tatu lazima yatazamwe,” alisema Lowassa.

Ibada katika Kanisa hilo, ambayo iliendana na harambee ya kuchangia hosteli na zaidi ya Sh89 milioni kupatikana, iliongozwa na Kaimu Askofu wa KKKT, Usharika wa Kaskazini Kati, Solomon Masango.

Katika mahubiri yake, Kaimu Askofu Masango alimtakia kila la heri Lowassa katika safari yake hiyo akisema anamtambua kuwa ni kiongozi bora.
Tags

Post a Comment

10 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. huyu jamaa akija kuwa rais, itakuwa ni mapenzi ya Mungu tu, lakini kwa upande wangu hana mfano mzuri, ndiyo ni mchapa kazi, lakini narudia, hana mfano mzuri hata kidogo kwenye jamii, wizi siyo mfano mzuri, Mungu ibariki Tanzania.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Alitoka uwaziri mkuu kwa scandals .sasa atarudije ?Mambo ya zuma .mwizi ni mwizi tuu

      Delete
  2. huyu aende cdm akaunga na sumaye chama kitakamilika

    ReplyDelete
  3. Ana roho mbayaaa na mkewe

    ReplyDelete
  4. Yes! Mr ila tunahofu usije ukawa kama wengine

    ReplyDelete
  5. MWIZI SANAAA HUYU.WAULIZE AICC CHANGANYA NA RICHMOND.HAFAIIIII

    ReplyDelete
  6. Shtuka mwananchi eee! Si alikuwa waziri huyu? Akatufanyia madudu.. Thn ananiuzi kutaka kujisafisha kupitia makanisani na misikitini, hana jipya ndio wale wale tu wanatunzungu, wananchi tunateseka, mi hata sikufikilii kukupa kura yangu.

    ReplyDelete
  7. nashukuru sana watanzania wenzangu kufunguka kuhusu huyu jamaa, kuna wengine bado wako kwenye usingizi, wanamshabikia sijui sababu ya hizo nywele nyeupe, huyu katuibia sana huyu, anachotaka ni kuja kuwa raisi ili alinde mali zake, zisiguswe.

    ReplyDelete
  8. hana mvuto amepoteza sifa

    ReplyDelete
  9. Huyu ni Oginga wa tanzania acha amwage hela zake maana anapunguza zile alizoliibia taifa zikiwemo misaada ya maafa alipokuwa waziri katika ofisi ya waziri mkuu enzi za waziri mkuu malecela.Tumwombe Mungu atuepushe na fisadi huyu namba Moja!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad