MSANII wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amesema kuwa sasa hivi anaiogopa na kuiheshimu sana pombe akiamini kwamba ndiyo chanzo cha maisha kuharibika.
Kwa mujibu wa tovuti ya GPL hivi , Lulu alisema tangu ametoka gerezani ameamua kujiweka pembeni na kilevi hicho na kwamba bora aitwe mshamba.
“Kiukweli nikiiona pombe kuna wakati naipa shikamoo kwani ndiyo kichocheo cha kila baya hapa duniani, watakaoniona mshamba kwa kubadilika kwangu wanione hivyohivyo,” alisema Lulu.
Msanii huyo kipindi cha nyumba alikuwa hakamatiki kwa kilevi na kuna wakati aliwahi kuzimika alipofakamia pombe za ofa alipokuwa ndani ya Ukumbi wa Maisha Club, jijini Dar.
LULU "NIKIONA POMBE HUWA NAIPA SHIKAMOO KWA JINSI ILIVYONIFANYA"
2
January 24, 2014
Tags
asante mungu nakuombea kwa mungu uzidi kubadilika mdogo wangu ukiwa na yesu akuna kinachoshindikana
ReplyDeleteHakuna kitu kizuri MTU jujitambua safi sana
ReplyDelete