Jambo limezua jambo! Mvua zilizonyesha na kusababisha mafuriko maeneo ya Dumila mkoani hapa, zimemuumbua mke wa mtu ambaye jina lake halikupatikana, akiwa anasaliti ndoa gesti.
Mafuriko hayo yalisababishwa na mvua kubwa zilizoanza kunyesha Jumatano iliyopita na kusababisha maafa makubwa yakiwamo kuharibiwa kwa makazi ya watu, majengo ya serikali zikiwamo shule, vyuo na mahakama.
Shuhuda wa tukio hilo, Lugendo Seleman, mkazi wa Kijiji cha Magole Tarafa ya Dumila Wilaya ya Kilosa mkoani hapa alimuonyesha mwandishi wetu gesti ambayo jamaa aliyefahamika kwa jina moja la Kashinde, mkazi wa kijiji hicho ambaye alikurupuka kuokoa maisha yake akiwa na mke wa mtu.
“Za mwizi kweli 40, Kashinde katoka gesti uchi wa mnyama na kupiga mbizi akiwa na mke wa mtu ambaye mumewe amesafiri muda mrefu yuko mjini akisaka maisha na ana kama miezi 6, huwa anakuja na kuondoa hivyo mkewe amekuwa na uhuru,” alisema Seleman na kuongeza:
“Umechelewa kidogo tu ungepata picha zao yeye na mke huyo wa mtu wakipiga mbizi uchi wa mnyama wakitokea gesti, sijui jana usiku walilewa sana mpaka wamechelewa kuamka na kukutwa na mafuriko, muda huu wa saa nne asubuhi!”
Aidha, juzi Alhamisi, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Waziri wa Ujenzi, John Magufuli walifika eneo hilo la tukio na kujionea hali halisi.
Akizungumza na wananachi wa Kijiji cha Magole, Pinda aliwaambia serikali imetoa chakula kwa waathirika wa tukio hilo na kuwataka wanachi kuwa wavumilivu katika kipindi hicho kigumu walichopitia.
MAFURIKO DUMILA YAMUUMBUA MKE WA MTU AKISALITI NDOA GESTI
0
January 26, 2014
Tags